Picha: Kwa mtu aliye mgonga Twiga kama hivi faini yake huwa bei gani?!

Picha: Kwa mtu aliye mgonga Twiga kama hivi faini yake huwa bei gani?!

Wakuu, naaamini humu kutakuwa na wajuzi watakaoweza kujibu swali langu hili.

Kama umegonga Twiga kama inavyoonekana hapo pichani, faini yake huwa ni shingapi?

Hii picha nimekutana nayo huko X na imenipa maswali mengi.

Na hiyo hela ukishalipa inaenda kwa familia ya Twiga kama fidia au inaenda wapi?

Dereva kazingua
 
Sasa million 40 ya kuijadili humu na nyie..? Watu wanagonga wake za wenye mamlaka sembuse twiga
 
Mtu aliyegonga na kuua twiga anatakiwa kulipa faini ya dola za kimarekani 15,000 ambazo ni sawa na takriban shilingi milioni 34 za Kitanzania.

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Ignas Gara, alisema hiyo faini kutokana na tukio la dereva wa lori aliyegonga na kumuua twiga katika hifadhi hiyo.
 
Aliyegonga wabunge zaidi ya 20 yeye vipi😕
 

Attachments

  • Screenshot_2024-12-06-10-29-13-966_com.instagram.android-edit.jpg
    Screenshot_2024-12-06-10-29-13-966_com.instagram.android-edit.jpg
    520.1 KB · Views: 3
Amos Nnko, Mkurugenzi ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafariki ajalini Same.
Huyu alipigwa fain Tsh ngapi??
 

Attachments

  • IMG-20241223-WA0017.jpg
    IMG-20241223-WA0017.jpg
    33.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom