Ulitaka wamtenge?! Una mawazo ya "KI-FARISAYO!"
Yesu hakufa msalabani kwa ajili ya watu "WAKAMILIFU" kama wewe, bali kwa ajili yetu "WATENDA MAOVU."
Unaikumbuka habari ya mwana mpotevu?
Yesu alikaa na watoza ushuru, wezi, makahaba, majambazi nk, ili awafundishe na kuwasaidia.
Kama mtawatenga wanaohitaji kuokolewa, neema ya wokovu wataipata wapi? Watasikia wapi Neno la Kristo ili waokolowe? Kwa sababu Imani huja kwa kusikia Neno la Mungu.
Hebu TAFAKARI maandiko haya;
"Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize. Mafarisayo na waandishi wakanung'unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao. Akawaambia mfano huu, akisema, Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone? Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi. Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea. Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu." - Luka 15:1-7
Ubarikiwe!