Picha: Mjengo Mpya wa Zamaradi Mketema

Kwa Dar hakuna porini, with time utashangaa yale maeneo yaliyodharaulika yanakuwa very potential. Barabara ya Tangibovu kwenda Mbezi kupitia Goba ilikuwa porini miaka hiyo, hakuna aliyefikiria kungekuwa na thamani kubwa, leo hii nenda kanunie kiwanja uone muziki wake, then jenga nyumba uone utapangisha kwa shilingi ngapi. Just imagine una two-bedroom apartments za kutosha kwa familia changa, one bedroom apartment kwa singles. Then njoo tujadiliane hapa.
 
Kina uwoya wa bize kuonesha tatoo,akishazeeka tutasikia anaomba michango akatibiwe India
 
Haha, sitaki kucheka kiongozi, its sad. Magu aliwaumiza wengi, kuna mmoja anaishi Kibamba kwa sasa, ukimtajia jina la Magu atatakukana hadi ushangae.
Acha tu mzee.....MAGU kaumiza watu sana pale kisa hawakumchagua.
 
Mkuu nyumba yangu ya kwanza nilimaliza 1990 Dar. Nakuomba ujue kuwa theory na practice ni mbingu na jua
 
Kama tumeweza kuona hapa tayari ni Show off! Umasikini kitu kibaya sanaa..
 
Wewe kijana mbona king'ang'anizi? Nyumba ni Liability na sio Asset, sawa sawa?
 
Nyumba nyingine ukijenga usitumie kokoto "UBUYU" nunua MSOLWA bei zake hazitofautiani sana.
 
Ni ardhi na siyo nyumba ambayo ni asset. Wengi wanaoongea kuwa nyumba ni asset, hawana au wanafananisha location kati ya kariakoo na buza.
Factor hapo ni ardhi/kiwanja. Kwa sie tuliorithi nyumba kadhaa, nakuhakikishia kuwa tumepata somo kubwa.
Hatuwezi kuishi kwenye hizo nyumba kwani maisha yangu si kama ya wazazi wangu.

Nyumba ya milioni 200 mnapangisha laki 2 kwa mwezi mpaka laki tatu.
Kurudisha hela ni miaka 80 mpaka 100. Hapo mshakufa.
Ila kama ukiweka milioni 200 kwenye hatifungani unapata zaidi ya mil. 25 kwa mwaka.
Na baba katuambia nyumba zake tusiuze na mashangazi wanatusisitizia hilo.
Bado huwa natamani ningerithishwa heka 10 madale au boko enzi hizo ilikuwa porini kuliko nyumba za temeke.
Trust me on this.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…