Picha: Mrembo Nyailong ambaye mahari yake ni ng'ombe 520 na magari 3

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Urembo wa binti huyo wa miaka 17 kutoka Awerial lililokuwa likiitwa Lake State Sudan Kusini umewashangaza wengi na hata matajiri wamejitokeza kuomba uchumba.

Kufikia mwisho wa Alhamisi, Oktoba 25, wanaume sita tayari walikuwa wameitembelea familia ya Nyalong Ngong Deng wakitoa ahadi za posa; mmoja wa wanaume hao anaongoza kwa kuwa tayari kutoa ng’ombe 520 naa magari matatu aiana ya Toyata V8.

Miongoni mwa wanaume wanaotafuta kumuoa msichana huyo ni aliyekuwa kamishna wa Awerial na Naibu Gavana wa Sasa wa Jimbo la Lakes State Mashariki. Kok Alat anaongoza katika kumtaka binti huyo hazikuwashtua wanaomfahamu kwa utajiri wake mkubwa katika mataifa ya Afrika Mashariki.

Ripoti zinasema kuwa, wanaume wengine zaidi wamejitokeza wakiwa tayari kuchomoa posa kwa ajili ya kumnyakua Nyalong.

Wanaume sita tayari wameonyesha utayari wao wa kuondoka naye.

Katika jamii ya Yirol, mwanamume yeyote anayetaka kuoa ni sharti kuwashawishi vilivyo wazazi wa msichana kabla ya kuruhusiwa,

Familia huwatathmini wanaume kadhaa kabla ya kuweka uwanja wazi kwa walioteuliwa kumposa msichana huyo.

Kwa sasa, bado pambano linaendelea na mshindi akipatikana, bila shaka tutawaarifu.

Screenshot_20181026-190843.jpeg
Screenshot_20181026-190920.jpeg
 
Urembo wa binti huyo wa miaka 17 kutoka Awerial lililokuwa likiitwa Lake State Sudan Kusini umewashangaza wengi na hata matajiri wamejitokeza kuomba uchumba.
Kufikia mwisho wa Alhamisi, Oktoba 25, wanaume sita tayari walikuwa wameitembelea familia ya Nyalong Ngong Deng wakitoa ahadi za posa; mmoja wa wanaume hao anaongoza kwa kuwa tayari kutoa ng’ombe 520 naa magari matatu aiana ya Toyata V8.
Miongoni mwa wanaume wanaotafuta kumuoa msichana huyo ni aliyekuwa kamishna wa Awerial na Naibu Gavana wa Sasa wa Jimbo la Lakes State Mashariki. Kok Alat anaongoza katika kumtaka binti huyo hazikuwashtua wanaomfahamu kwa utajiri wake mkubwa katika mataifa ya Afrika Mashariki.
Ripoti zinasema kuwa, wanaume wengine zaidi wamejitokeza wakiwa tayari kuchomoa posa kwa ajili ya kumnyakua Nyalong.
Wanaume sita tayari wameonyesha utayari wao wa kuondoka naye.
Katika jamii ya Yirol, mwanamume yeyote anayetaka kuoa ni sharti kuwashawishi vilivyo wazazi wa msichana kabla ya kuruhusiwa,
Familia huwatathmini wanaume kadhaa kabla ya kuweka uwanja wazi kwa walioteuliwa kumposa msichana huyo
Kwa sasa, bado pambano linaendelea na mshindi akipatikana, bila shaka tutawaarifu.

View attachment 912021View attachment 912022
ila kweli mrembo hana uzuri wa dukani wala wigi...ni kifaa original...
 
Huyu ni "kigori" hasa, kipusa wa nguvu, huyu ni "mwali" hasa, nikisema ni mwali, maana yake hajaguswa bado na mwanaume yeyote. Huyu mtoto ni "mzuri" sana, isipokuwa tu hawa watu wa Sudan huwa wanawakeketa hawa watoto.
 
Back
Top Bottom