"unafikiri nchi hii inaendeshwa na wendawazimu?mkusanyiko wa watu wengi sio ushindi wa chadema kwani kuna watu wanaenda kumsanifu tu slaa kwa ahadi zake za uongo.we unafikiri chama kipya kikitawala nchi hii kutakuwa na maendeleo?si wao watataka kushibisha matumbo yao kwanza na watu wote waliyo wa support ndio watufikirie mimi na wewe na kibaya zaidi watu wanayo support chadema ni wachaga,daima hawashibi.muwe mnafikiria mnacho zungumza,sio upambe tu.unapo zungumzia kodi,sikazi wewe haujawahi kulipa kodi toka uzaliwe.tuache ushabiki,tuangalie ukweli"
Bwana Shida Mwadila!! Kama utaniazima muda wako kidogo tu wa kusoma na kuelewa mambo haya, nadhani utabadilika sana kifikra.
Ni kweli nchi haiongozwi na wendawazimu, lakini ukifanya mambo yanayopingana na maadili pia ni kama uendawazimu. Fikiria mtu mwenye akili timamu akiamua kuvua nguo sokoni mchana kweupe ataonekanaje? Je, inakujia akilini mtu mzima aliyeelimika, anaetambua sababu za maambukizi ya ukimwi kwa mwanadamu, akawaambia wote waliopata maambukizi hayo ni kiherehere chao. Ni kwa namna gani mtoto azaliwaye na ukimwi amepata kwa kiherehere chake? Kiongozi bora ni yule anayetenda anachokiamini na kukisimamia, si yule anayenena asichotenda.
Umati wa wananchi wanaoenda kumsikiliza sio kielelezo tosha cha ushindi kama ulivyosema, lakini ni ujumbe kwamba watu wana imani nae na pia kuwa kuna tatizo katika utawala uliopo.
Kushibisha matumbo kwanza ni dhana uliyonayo wewe, sidhani ndio msingi wa uongozi wa nchi, kama ndio utamaduni uliozoea, basi huna budi kubadilika. Si viongozi wote wenye mtazamo wa kujilimbikizia mali wao kwanza, rejea jimbo la karatu utapata majibu pale.
Chama cha wachaga!!!! Ndugu yangu hizo ni propaganda chafu za CCM, kututenga kwa kutumia ukabila, udini na tofauti nyingine. Kama uchaga ni uenyekiti, je, CCM ni chama cha wakwere? (JK, Salma, Ridhwani n.k au family party?)
Unapojenga hoja tafakari na tumia hoja zinazoishi na si hoja zahania.