Bandugu mbona hiyo picha mimi siioni, au ndiyo wamechomoa tayari?:whistle:
Duh, hata mimi sizioni hizo picha...
Jamani kwangu haifunguki, sijui hawa jamaa wameshaipiga pini? Natamani kujua yaliyojiri jana huko Ng'wanza.
Hizi picha ni zilezile zilizopita yaani siku zote jamaa anapigwa picha akiwa anaangalia mkono wa kushoto ,mnachakachua lakini muwekeeni chunvi na sukari karibu hapo tarehe mbili ambapo matangazo yatatangazwa rasmi.
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake, katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana kwenye uwanja wa Magomeni, Kirumba.
