MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Analytical mind yako uwa mega smart lakini wakati mwingine ujisahau na kuwa fyatu kidogo - chukulia mfano wa wewe kuanza kuwabeza Watanzania eti tunajifanya raia wa South Afrika ni ndugu zetu, labda nikukumbushe historia ya nyuma - ni hivi mkuu: Watanazia maelfu walimwaga damu yao wakipigana bega kwa bega na ndugu zetu wa Afrika kusini kukomboa Taifa lao lililo kuwa chini ya makaburu, swali ni ,je, Kenya/Kenyatta alitoa mchango gani kuwakomboa Waafrika wenzao dhidi ya ukoloni specifically in Southern Africa Region, tuwe wakweli hapa Kenyans contributed nothing , sana sana walikuwa wakishirikiana na makaburu wenyewe na Ian Smith kuchelewesha ukombozi kusuni mwa Afrika, wanashirikiana na Chester Croker, Voster/Botha na so called Constructive engagement designed kuchelewesha uhuru Afrika Kusini pamoja na majirani zake.
Linapo kuja suala la Serikali ya Kenya ya wakati huo kusaidia ukombozi wa Waafrika wenzao barani Afrika - Kenya was and still is a disgrace - akili zao zote zipo kwenye kutafuta mbinu za kufanya biashara na kujaribu kuziibia big time na alaghai juu mataifa ya kusini mwa Afrika - kazi kujifanya wao wana akili sana kuliko Mataifa mengine barani Afrika wanafikiri waafrika bado wamelala usingizi - ndio mlivyo, man eat man vitu vingine kwenu ni secondary mmekubuhu kwenye wizi, ulaghai na kufiti yaifa na taifa ili watu wasielewane, roho ya kutu ndio uwasumbua sana sijui kwa nini?
Sio kwamba nawasingizia mbona mifano hipo mingi sana ya ku-support maoni yangu juu ya unafiki wenu uliyo pitiliza mipaka, la kwanza: Mliwahi kuvalia njuga suala la ujenzi wa barabara kupitia mbuga za wanyama nchini mwetu - hamkutaka barabara hiyo ijengwe, mkapeleka malalamiko yenu mpaka kwenye jumuhia ya kimataifa mkidai eti Tanzania inaingilia eco systems za mbuga za wanyama kwenye hifadhi ya Serengeti na Ngorongoro - ulaghai mtupu.
Hamkuishia hapo, siku nyingine mkatushitaki kwenye hizo hizo jumuhia za kimataifa eti Tanzania inauwa tembo wengi hivyo wasiruhusiwe kuuza meno ya tembo kwenye mnada,mnaisema Tanzania huku Afrika Kusini na Zimbabwe zinaruhusiwa kuuza meno ya Tembo kimataifa - siku nyingine mkailalamikia Dunia eti Tanzania inazuhia Nyumbu ku-cross mto Mara na kwenda kwenye hifadhi yenu ya Masai Mara - akili gani hizi kama sio kuchanganyikiwa, mwisho ni hili suala la ujenzi wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme huko mto wa Rufiji, na hapo mlisha anzisha chokochoko zenu eti ujenzi wa bwawa hilo utaharibu mahekta na mahekta za misitu na wanyawa kukosa pa kuishi hivyo ingekuwa vyema kama mradi huo ungesitishwa - hizi kama sio akili za kichawi tuziiteje?
Now back to the main point: ukombozi barani Afrika, kama nakumbuka Rais Zuma wa Afrika Kusini pamoja na Mugabe wa Zimbabwe waliwahi kuisuta Kenya live kwamba hakuwahi kusaidia chochote katika harakati za kuwakomboa Wafrika wenzao dhidi ya ukoloni kusini mwa Afrika - lakini cha ajabu Kenya hiyo hiyo ndio inataka ipewe kipa umbele katika uwekezaji kwenye Maitaifa yaliyo kombolewa na Tanzania,Zambia na Msumbiji - Zuma na Mugabe walisema hawataki kuwasikia Wakenya wakija nchini mwao wakijifanya ni wawekezaji yaani wanataka kuvuna ambacho hawakuwai kukipanda - wenzao walimwaga damu kukomboa Afrika Kusini na Zimbabwe wakati huo Kenya ilikuwa kimya kabisa ie waliona masuala ya Ukombozi haya wahusu kabisa save wakenya kutaka ku-invest kwenye mataifa yaliyo kombolewa na wenzao kwa mtutu wa bunduki hata aibu hawana kabisa.
Liinsha lote hili siku ya wiki, subiri nitalisoma na kukujibu nikipata fursa, nimepita juu juu tu na kuona ni zile yada yada za mliikomboa Afrika ambazo ni ngonjera zisizo na mantiki enzi za leo, watu wanapambana na umaskini, hiyo Afrika kusini vijana wa leo wanahangaika kwenye soko la ajira, wengi hawamjui Mandela, humskia tu ila hawana muda huo wa nyimbo za uzalendo wakati nchi yao ufisadi umetamalaki akina sijui Zuma wanaiba na kuoa wake wengi ukihoji unaambiwa Mandela aliikomboa nchi.
Ndio hata kama ilivyo Tanzania, vijana wenu wanahangaika kwenye umaskini na ufisadi ila wakihoji mnawajibu na hizi pumba za sijui Nyerere aliikomboa Afrika.