Pre GE2025 Picha: Nape Nnauye atua mtaani akiwa na nguo za kiraia huku akila ubwabwa na wananchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu ni 2025 hii. Muda wa publicity huu

Na sisi watanzania tunapenda kumasajiwa kihisia ili tuone nasi twajaliwa na hao "watoto wa wakulima wastaafu"..

I never thought the phrase "emotional massage" was a thing until i read your comment 😂😂
 
Kwa hiyo anaamini hayo ndo mahitaji ya Wananchi?
Ndiyo jinsi ya kuwakamata Wabongo and that's what matters most. Kazi ya kuwapatia wananchi mahitaji haimuhusu kwa sasa, yeye ana majukumu ya kuwawakilisha bungeni wapiga kura wake.
Serikali ndiyo inapaswa kuhakikisha wananchi wanapatiwa mahitaji yao, Nape is not in the government for now.
 
Alafu mnene n yeye tu...!!!
 

Mkuu, that is not my job.

Kama amepeleka maji huko kwenye hivyo vijiji, well and good. Ndio anacholipwa kufanya, its his job.

Hajitolei huyo analipwa kwa kodi yako. Au ulitaka tumuimbie mapambio kwa kutimiza wajibu alioahidi kufanya?

Sisi tutafocus kwenye sehemu ambazo hajapeleka huduma za maji.

Ni aibu huyo baba yuko very close na mawaziri anashindwa ku-lobby Mtama yote ikapate maji instead yuko bize kula ubwabwa na ccm wenzie

Siku akiepeleka maji kwenye vijiji vyote mtama rudi hapa like hii comment. Nitakujibu!
 
Nguo za kiraia! Ulitaka avae nguo gani huyu division four?

Angevaa yale masuti yao wanayovagaa wakati wa kuapishwa au wakialikwa kwenye "tafrija" za wasanii wa CCM.

Nape sio wa kuvaa Ma Tshirt ya Foma Gold.

Kuhusu Division Four nilikuwa sijui.

Kamaliza shule gani huyu baba?
 
Hapo ni kambini sio sehemu tu ya mnavyoongea sijui wananchi. Acheni kuropoka fatilieni. Sio kitongoji hiko. Watu wanafuliwa hapo
 
Kwa hiyo anaamini hayo ndo mahitaji ya Wananchi?
It doesn't matter, na wapiga kura wake hawajali. Baada ya huo ubwabwa watampigia kura za ndio. Akichanganya na mbinu chafu, anashinda ubunge, maisha yanaendelea. Hii ndio Bongoland.
 
Ukishajua akili za wapiga kura wako wala haisumbui, msimlaumu Nape Nnauye kwani anayoyafanya mbele ya lenzi za kamera ni reflection ya akili na mahitaji ya wapiga kura.

Njaa Yao Iko tumboni hawahitaji barabara, huduma za afya, elimu, miundombinu au nishati.

Wao wanaona ubwabwa ni kazi kubwa kaifanya mheshimiwa mbunge.

Matatizo ni Yale Yale kila mwaka wa uchaguzi na ahadi ni zile zile!
 
Nguo za kiraia kwani yeye huwa anavaa sare za aina gani!
 
Kwa hiyo anaamini hayo ndo mahitaji ya Wananchi?
Mkuu Nape anatimiza jukumu lake la msingi la kibunge kwa kukutana na wapiga kura wake, kuchangamana nao na kuongea nao kama sehemu ya kupokea maoni na kero zao ili aziwazilishe bungeni kama mwakilishi wao.
 
Hii mbona kawaida Sana wananchiwapiga kura wameshaanza kutongozwa
 
Huyu jamaa kwa sababu ya kiburi na jeuri zake huwa namchukia hapo,
Ila nasikia nasikia huu mwaka yeye anainuliwa tena,

Ila kiburi mwenzake Makamba ni mwaka wa kuomboleza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…