Picha:-Ni tunda /Chakula gani cha Asili ambacho unakipenda zaidi?.Nitakuambia baadhi ya faida ya matunda hayo

Picha:-Ni tunda /Chakula gani cha Asili ambacho unakipenda zaidi?.Nitakuambia baadhi ya faida ya matunda hayo

FB_IMG_1740089795859.jpg
 
View attachment 3243461
Hapa nitie neno kidogo.Sijui kiswahili inaitaaje hii type ya mapishi but kisukuma huitwa shibhongote.

Shibhongote mara nyingi walikuwa wanapikiwa watoto na wazee wasikuwa na meno.

Process ilikuwa ni hivi......

Unachuma mahindi ambayo hayajakomaa sana Kisha unaponda(twanga) au kama ni muhongo unafanya vile vile.

Baada ya hapo unafunga kwenye majani ya mgomba namna hiyo kwenye picha Kisha unachemsha kwenye maji hasa ukiwa unachemsha mahindi/viazi yenyewe unaweka juu kabisa inaiva na mvuke tu.

Kwa Sasa unaweza ongeza utundu kwa kumix Aina kadhaa wa kadhaa. Chakula kizuri sana kina ladha nzuri na pendant sana kwa watoto tumia mahindi machanga kiasi ndo matamu halafu usitwange wee tumia Brenda!!
Huku niliko yanaitwa MABOBWE. Wanatumia unga wa ngano, sukari na chicha kidogo nadhani na iliki (hiliki).
 
Papai nampenda mno, na fenesi na parachichiii
Faida za fenesi mwilini


Kinga dhidi ya magonjwa​

Fenesi ni chanzo muhimu cha aina mbalimbali za phytonutrients, misombo hii ya mimea ni kinga na inayoweza kusaidia kuzuia maendeleo ya baadhi ya magonjwa sugu, kama vile kisukari. Ina vitamini C, carotenoids pamoja na polyphenols na flavonoids.
Hutumika katika matibabu ya saratani ya tezi dume, saratani ya tumbo, saratani ya mapafu, magonjwa ya moyo na shinikizo la damu. Pia ina uwezo wa kuzuia mtu kuzeeka.

Inaweza kusaidia kuboresha afya ya moyo​

Pamoja na kusambaza phytonutrients ya kinga fenesi pia ina virutubisho rafiki kwa moyo ikiwa ni pamoja na potasiamu na nyuzi.

Chanzo cha vitamini na madini.​

Fenesi ina kiasi cha chini cha kalori wakati, kulingana na angalau utafiti mmoja ina virutubisho vingi zaidi kuliko matunda mengine mengi maarufu kama vile tufaha, parachichi na ndizi. Kwa kweli, mbegu na nyama yake ina kalsiamu na chuma zaidi kuliko matunda mengine ya kitropiki na ni chanzo muhimu cha vitamini B ikiwa ni pamoja na B1, B3, B6 na folate.

Kuboresha kinga ya mwili.​

Ni viungo vya nyuzi katika tunda hili zinazosaidia utumbo pamoja na vitamini C na beta-carotene ambayo yanapendekeza kwamba fenesi inaweza kusaidia afya ya kinga na uwezekano wa kupunguza hatari ya kuambukizwa na virusi.
Mbali na hayo, kiungo kilichopatikana katika mbegu ya matunda kinaonekana kuamsha seli muhimu za kinga, zinazoitwa neutrophils. Seli hizi za kinga ni mojawapo ya mistari yetu ya kwanza ya ulinzi na huongeza nguvu za seli nyingine za kinga.

Kutengeza bidhaa nyingine​

Kando na kutumika katika kuoka na kutengeneza sharubati na saladi. Fenesi inaweza kupikwa ikiwa kijani. Mbegu zinaweza kupikwa au kuliwa zikiwa mbichi.
Pia fenesi hutengeneza Pipi, ice cream, juisi, mvinyo , jamu, na kachumbari.
Majani yake hutumiwa kwa kawaida kulisha mbuzi na ni chanzo kizuri cha protini na nguvu.
 
Back
Top Bottom