Papai nampenda mno, na fenesi na parachichiii
Faida za fenesi mwilini
Kinga dhidi ya magonjwa
Fenesi ni chanzo muhimu cha aina mbalimbali za phytonutrients, misombo hii ya mimea ni kinga na inayoweza kusaidia kuzuia maendeleo ya baadhi ya magonjwa sugu, kama vile kisukari. Ina vitamini C, carotenoids pamoja na polyphenols na flavonoids.
Hutumika katika matibabu ya saratani ya tezi dume, saratani ya tumbo, saratani ya mapafu, magonjwa ya moyo na shinikizo la damu. Pia ina uwezo wa kuzuia mtu kuzeeka.
Inaweza kusaidia kuboresha afya ya moyo
Pamoja na kusambaza phytonutrients ya kinga fenesi pia ina virutubisho rafiki kwa moyo ikiwa ni pamoja na potasiamu na nyuzi.
Chanzo cha vitamini na madini.
Fenesi ina kiasi cha chini cha kalori wakati, kulingana na angalau utafiti mmoja ina virutubisho vingi zaidi kuliko matunda mengine mengi maarufu kama vile tufaha, parachichi na ndizi. Kwa kweli, mbegu na nyama yake ina kalsiamu na chuma zaidi kuliko matunda mengine ya kitropiki na ni chanzo muhimu cha vitamini B ikiwa ni pamoja na B1, B3, B6 na folate.
Kuboresha kinga ya mwili.
Ni viungo vya nyuzi katika tunda hili zinazosaidia utumbo pamoja na vitamini C na beta-carotene ambayo yanapendekeza kwamba fenesi inaweza kusaidia afya ya kinga na uwezekano wa kupunguza hatari ya kuambukizwa na virusi.
Mbali na hayo, kiungo kilichopatikana katika mbegu ya matunda kinaonekana kuamsha seli muhimu za kinga, zinazoitwa neutrophils. Seli hizi za kinga ni mojawapo ya mistari yetu ya kwanza ya ulinzi na huongeza nguvu za seli nyingine za kinga.
Kutengeza bidhaa nyingine
Kando na kutumika katika kuoka na kutengeneza sharubati na saladi. Fenesi inaweza kupikwa ikiwa kijani. Mbegu zinaweza kupikwa au kuliwa zikiwa mbichi.
Pia fenesi hutengeneza Pipi, ice cream, juisi, mvinyo , jamu, na kachumbari.
Majani yake hutumiwa kwa kawaida kulisha mbuzi na ni chanzo kizuri cha protini na nguvu.