nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,801
- Thread starter
- #21
Kwamba hoja yao ilikuwa ni Watanzania kutoka kona mbalimbali; SIDHANI! Hoja ya Wapinzani ilikuwa ni namna ya kuwapata wale wabunge wa ziada (mbali na hawa sasa!) Kwamba, wakati utaratibu uliowekwa ni kwamba hao wa ziada (about 300) watateuliwa na Rais baada ya kuwa ameletewa majina matatu! Kwamba, SAY Jamiiforums ingekuwa nasi tunataka mwakilishi wetu, basi sisi wenyewe tunachagua/tunateua majina matatu na kuyapeleka IKULU kisha JK anateua moja kati ya hayo matatu! Hii ndiyo hoja ya msingi; hususani kwa CHADEMA! Haya ya kwamba Wazanzibari hawakushirikishwa ni porojo tu za kisiasa....anyway, this's like war; no war without propaganda! Hawakuosea kuleta suala la kutoshirikishwa Wazanzibar ili kutafuta uungwaji mkono!
So, vyama vya upinzani hawoni kama ni sahihi kuachia JK kuteu hao watu! Hofu yao ni kwamba, baada ya majina kupelekwa IKULU, huenda wana-mikakati wa CCM waka-scrutinize na kujua kwamba among the Three Names brought foward; X and Y wanweza kutetea maslahi ya CHADEMA wakati Z anaweza kutetea Z na hivyo Mkulu akakata shauri la kumteua Z!! Katika stahili; ikiwa wanachanga karata sawa sawa; basi si ajabu out of (say) 300, basi 200 wakaenda Mjengoni kutetea maslahi ya CCM na hivyo ukichanganya na wale waliopo; CCM wakawa na mtaji wa angalau WATETEZI 400 huku 200 wakienda pale kutetea upinzani (CHADEMA?) Nafahamu, huku mitaani watatupiga fix kwamba ni Katiba ya Watanzania lakini Si mwanachama wa CCM wala CHADEMA ambae ataweka maslahi ya Watanzania kwanza!
Sasa basi, issue ipo hapo kwenye kuwapata hao wabunge; itumike njia gani? Ikumbukwe kwamba wanaohitajika kutoka kwenye hivyo vikundi ni takribani wabunge 300 wakati taasisi husika zipo zaidi ya mia tatu!! SWALI: Kama idadi ya taasisi/NGOs, CBOs ni kubwa kuliko idadi ya wabunge wanaohitajika; Sasa kama uteuzi ufanyike kutokana na hoja ya Upinzani; kwanini ni Taasisi A ndiyo iwe na mwakilishi na sio B? By the way, ni nani huyo atakayeteua hiyo taasisi A itakayotoa mwakilishi? Sina uhakika kama nimeeleweaka; assume kuna CBOs/NGOs/and the Like 400 ambazo collectively wanatakiwa kupeleka wawakilishi 300; so, ni nani huyo atakayechagua taasisi 300 out of 400? Tuamini kwamba hawa watakutana kisha wakapiga kura? Anyway, sisemi kwamba haiwezekani inawezekana kabisa lakini ninachotaka kusema ni kwamba WAPINZANI WAMEPIGWA CHANGA LA MACHO! JK alichowakubalia ni kwamba hoja irudi Bungeni! Siamini kwamba CCM wata-vote against exclusive right ya President katika kuteua mtu mmoja out of the THREE! Unajua itakavyokuwa?
Itakuwa hivi; baada ya mjadala mkali, hatimae kura zitapigwa! Wanaosema ndiyo; NDIYOOOOOOO, wanaosema siyo; SIYOOOOOOO! Mnyika atasimama tena na kusema tuhesabu kura moja moja na mwisho wa yote Waliosema NDIYOOOOOO (CCM) wameshinda! Hapo sasa; CHADEMA na wenzao wakitoka tena ukimbini; wataonekana KUMBE KWELI CHADEMA WAKOROFI! Rais amewasikiliza; hoja imerudishwa bungeni; Wengi wameamua lakini BADO CHADEMA HAWATAKI!
Ole wao ambao wanaomwa-undermine JK!
Kama watachaguliwa RANDOMLY na JK sio tatizo sababu watu hao watakuwa huru kujadili hiyo KATIBA; Sidhani sababu RAIS kaniteua nitampa atakacho sijui Rais anataka nini kwenye KATIBA...