Picha: Rais Samia akiwa kwenye kiwanda cha Volkswagen nchini Rwanda


..trillion 2 zilizotumika kununua ndege ni sawa na bajeti ya wizara ya kilimo kwa miaka 6.

..Na kilimo ndicho kinachoajiri watu [ 65% + ] wengi hapa Tz. Pia tumekuwa tukiambiwa ndio uti wa mgongo wa taifa letu.

..Kauli mbiu ya serikali ya awamu ya 5 na 6 ni Tanzania ya VIWANDA.

..Na viwanda hivyo vinatakiwa vitumie malighafi zinazotokana na wakulima wetu.

..Kwa msingi huo, ni lazima tukiinue kilimo chetu ili tuweze kuzalisha mazao mengi na yenye ubora wa kuweza kutumika kama malighafi ktk viwanda tunavyotarajia vitaanzishwa.

..Njia ya uhakika ya kuinua kilimo ni kuongeza bajeti inayokwenda ktk sekta hiyo kusaidia ktk huduma za ugani, utafiti wa mbegu bora, upatikanaji wa pembejeo, etc etc.

..Nchi yetu na watu wake ni masikini kwasababu serikali zetu zote hazikuwekeza vya kutosha ktk kilimo, ufugaji, na uvuvi.

..Tatizo la shirika la ndege haliko ktk usimamizi bali liko ktk changamoto na ugumu wa biashara ya usafiri wa anga. Hata tukiweka malaika kuongoza shirika letu la ndege bado tutaingia hasara.
 

Sahihi
 
Nafikiri hoja yako iwe ya pili, ya kwanza kwanini kanchi kadogo kama Rwanda ambako hakana ardhi kubwa ya kilimo, hakana bandari, hakana madini na NP kama Tz kanatuzidi kimaendeleo?
 
Reactions: Qwy
Nafikiri hoja yako iwe ya pili, ya kwanza kwanini kanchi kadogo kama Rwanda ambako hakana ardhi kubwa ya kilimo, hakana bandari, hakana madini na NP kama Tz kanatuzidi kimaendeleo?
Ukubwa wa pua si wingi wa kamasi, look at Switzerland.
Kagame akili kubwa, rais mwingine kichwa ni Uhuru Kenyatta.
 
Unajuaje kama aliyeandika comment hiyo ni kijana, inawezekana akawa amemzidi umri huyo bi Mwenda wenu.
Mtu mzima hana majibu kama yako na huyo kijana mwenzio
Kwa maana hiyo hata mama yako mzazi nae bi Mwenda?
 
Kuna mengi ya kujifunza kutokea Rwanda. Jeshi la Rwanda limepata mafunzo na kuboreshwa hivi sasa linatumika kama chanzo cha mapato ya nchi kwa kulinda usalama kwenye sehemu zenye migogoro na pengine kutumika kwenye mapambano kama ilivyo sasa huko CAR na Mozambique.

Jamaa Pamoja na kuitwa dikteta anaongoza watu wanaojitambua wenye lengo la kuifanya nchi iwe kwenye chati za juu. Mikakati iliyonayo Rwanda kama taifa ikifanikiwa miaka kumi ijayo tutabaki midomo wazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…