Picha:Tajiri namba moja lakini anaishi kawaida kabisa

Picha:Tajiri namba moja lakini anaishi kawaida kabisa

Mleta mada bado sijamuelewa, sasa hii picha ndio inaonyesha maisha yake anaishi vipi?
 
Mimi nilifikiri anaishi kwenye nyumba ya kupanga na hata akipanda ndege hupanda daraja la economy!!! au anatembelea vitz !!!Kumbe unafikiri anaishi kawaida kwasababu ya muonekano wake ... duh,jipe moyo mpo sawa.
 
8434958c50a742f8aaa1c18337011fa2.jpg


a53e3cd8603021581f7a051d6b2a90d7.jpg


29dc2360ff4a26a4b8facb4cfeccab9d.jpg


[emoji115] Steve Jobs CEO wa Apple.
Billionaire lakini ukimtizama au kukutana naye utadhani ni mzee anayeshinda kwenye vijiwe vya kahawa yupo simple .

Sasa ww ukipata vi laki 3,5 zako kila mtu atajua utajishebedua,gari ulikimbize ututimulie mivumbi
[emoji15] [emoji15] [emoji15] yuko simple aseee
 
Pembe la ngombe halifichik.....pamoja NA mgaun wote huo ila bado vitu adimu vinaonekana
 
Hata Warren buffet ana live large, anajinafikia tu kwenye media kwamba he is frugal, its pointless kuwa na mabilioni ya dola hlf uishi kimaskini labda hela ziwe za masharti Tyta
ha ha mkuu maisha ya kimasikini ni yapi kweni? ukiwa tajiri huwezi kuishi maisha ya kimasikini by any means, lazima tu utaishi maisha ya kitajiri
 
Ungetenganisha hizo picha ili Dangote aonekane...hapo Mtu unaangalia macho yanavutwa kushoto.
 
*Iko hivi*

“Maskini na tajiri wana mawazo tofauti.

Maskini hudhani utajiri ni chanzo cha matatizo.

Tajiri hudhani umaskini ni chanzo cha matatizo.

Maskini hudhani ubinafsi ni kitu kibaya.

Tajiri hudhani ubinafsi ni kitu kizuri.

Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi.

Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi.

Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa.

Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake.

Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda.

Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda.

Maskini hudhani kuwa tajiri lazima usome sana.

Tajiri hudhani kuwa tajiri si lazima usome sana.

Maskini hutamani mambo mazuri ya wakati uliyopita.

Tajiri hutamani mambo mazuri ya wakati unaokuja.

Maskini huamini ili uwe tajiri lazima ufanye kitu fulani.

Tajiri huamini ili uwe tajiri lazima uwe kitu fulani.

Maskini hupenda kuburudishwa kuliko kuelimishwa.

Tajiri hupenda kuelimishwa kuliko kuburudishwa.

Maskini ana woga.

Tajiri hana woga.

Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha.

Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri.

Maskini hana nidhamu ya mapato na matumizi.

Tajiri ana nidhamu ya mapato na matumizi.

Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa.

Tajiri hutumia pesa kupata pesa.

Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake.

Tajiri ni mkubwa kuliko matatizo yake.

Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa.

Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine.

Maskini ana wivu wa chuki. Tajiri ana wivu wa maendeleo.

Fikiri kama anavyofikiri tajiri.

Ukifikiri tofauti na anavyofikiri tajiri, utakufa maskini.”

Chanyata Ubongo wako sasa!
Umetisha
 
Labda Ana utajir wa mashariti,weng wenye utajir wa uchaw wanaish kawaida wengine wanavaa had nguo zilizochanika
 
Back
Top Bottom