Kwa mm ambae nimewahi kufanya kazi SBL kitengo cha maintenance hakuna shida, Kuna factor nyingi zinasababisha chupa kuwa na ujazo tofauti, kwa sababu machine nyingi zinazojaza huwa pneumatic system, kiasi kwamba upepo ukipungua panakua na variation ya ujazo kotoka chupa na chupa, kipindi Quality control wanakagua baadhi ya chupa huwapita.
Kuhusu lebo inategemea na supplier Kuna kipindi supplier hatoi mzigo wenye quality mnayoitaka. Kwahio kama lebo zimeisha hulazimika kutumia lebo zilizopo hata kama hadhikidhi ubora. Ili mradi mzigo ufike kwa mteja, na wateja hufahamishwa juu ya mabadiliko hayo.
Sasa kuhusu ni fake au si fake wakuthibitisha ni mamlaka zinazohusika. Lakini pia Kuna kipindi wapishi wenyewe hutoa bidhaa isiyo na ubora kwa kukosea baadhi ya ratio katika uchanganyaji na kutokupata radha stahiki iliyotarajiwa na mzigo huwa unachanganywa na batch nyinginezo Ili kuepuka hasara.
Yote kwa yote epuka unywaji wa Pombe ni hatari kwa afya yako.