Uchaguzi 2020 Picha: Ukumbi wa Mlimani City ukiwa tayari kwa Vikao vya Maamuzi CHADEMA kuanzia kesho, taratibu za kujilinda na COVID-19 zimezingatiwa

Asante Sky Eclat Je hizo hoteli/gesti za sinza unaweza kwenda mpaka mlimani kwa mguu au itahitaji bodaboda maana mie kutembea mwendo mrefu siwezi. nitashukuru ukanipa jina la hoteli iliyo karibu sana na mlimani city.
Unaweza kutembea kwa miguu, Kuna bajaji na boda boda za kumwaga
 
Waweke ulinzi Cyprian Musiba na magaidi wenzake wasijetega mabomu maana akili ya ni kumwaga damu tu kama alivyokuwa anatamba.
Usiwe na shaka hawa jamaa sio kama sie.
Hawana taaluma ya kupiga risasi 16 na zote zikaukwepa mguu wa kushoto na kupiga kona zilipomkaribia dereva ili kugeuka kutungua mguu wa kulia wa mzee wetu wa MIGA.
Hii taaluma ipo kwetu tu! maCCM hayana.
Ndo maana hadi sasa hayaelewi dereva aliponaje wakati mguu wa kulia wa mzee wa ACCACIA ulikuwa upande wake?
 
Ndugu makamanda na wanachama wa Chadema tukio zima la kikao pale mlimani city litarushwa mubashara na Barmedas Tv. Kwa wale wa Startimes iko channel no 115.
 
Wakuu sijui kwanini moyo wangu unakuwa mzito hivi, nina wasiwasi hawa wajumbe hasa mikoani wanaweza kupindua meza wakampa Nyalandu.

Aisee ikifika stage hiyo ni heri udikteta utumike wakuu apite Lissu kipenzi cha watanzania.
Usiwe na hofu Kamanda, game lilishaisha kitambo na kinachoenda kufanyika ni kuwekwa record sawa.

Lissu na Nyalandu wapo pamoja na baada ya uchaguzi huu Nyalandu atashiriki kwa nguvu zote kuakikisha kura za Lissu zinatosha
 
Makada wa CCM nawaona nawaona,
wajumbe wa CDM ni makatili sana kuliko wale wa CCM.

Utawanunulia Bia watakunywa,
nyama choma wakula na mkeo watamgonga mande but kura watakuwa 0 🤣🤣
Nyalandu atapita kwa 100%
 
MLIO MLIMANI CITY TUNAOMBA UP TO DATE ZA JTATU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…