PICHA: UNAHITAJIKA MKAKATI WA KUSAFISHA FUKWE ZA DAR NYINGI NI CHAFU SANA

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Niko napiga jalamba humu beach ya Mbezi Beach kwa kweli hizi FUKWE ni chafu sana. Ni bahati mbaya pia kwamba hizi ndio FUKWE zilizopo ukanda wenye Mahoteli ya Kitalii kama vile White Sands, Ramada, The Waves, Landmark nk....Mkuu wa Mkoa wa Dar hili ni la kulivalia njuga kama mlivyofanikiwa Coco Beach.

Hii inakwaza pia ukuaji wa utalii Dar. Uchafu hauvutii utalii wa FUKWE na eneo hili Lina beaches nzuri sana ila chafu sana.
 
Fukwe zetu ni mali ya umma! Baadhi ya fukwe zinazomilikiwa na mahoteri binafsi ni safi sana! Mfano wet&wild, whitesand, silversand. Sasa beach za cocobeach ni cha wote!
 
Yaani tuache kupambania ugali tukasafishe beach! Acha bahari ijisafishe yenyewe, maana hiyo kazi inaiweza. Ipo siku hata lami mtapendekeza zidekiwe kisa kuna matope wakati mvua ipo na itasafisha tu automatically, ni suala la muda tu.
 
Inakera watu kwao pasafi afu unakuta mifurushi/viroba vya taka vimetelekezwa nyuma ya fensi au eneo lako
 
Uchafu ni maplastiki, sasa hayo mabaki ya mimea unaita uchafu?
 
Mamlaka husika wawajibike. Huu ni uzembe kupitiliza
Wawajibike wasafishe fukwe chafu sana.

Watafute wadau kama walivyofanya Coco.

Uchafu mbele ya mahoteli ya 4 5 star haifai kabisa wageni wanaweza kusambaza maneno yenye athari...si unajua wanapenda fukwe safi kama Zanzibar.
 
Huo sio uchafu mzee unataka beach zote zimilikiwe na matajiri ss makabwela tutainjoy wap
 
Hata wakisafisha bado raw sewage inaingia baharini kila dakika. Ni beach zisizofaa kabisa.
 
Hata wakisafisha bado raw sewage inaingia baharini kila dakika. Ni beach zisizofaa kabisa.
Beach zinasafishika, hiyo raw sewage CocoBeach wamemudu vipi kuiondoa mbona hizo beaches zina usafi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…