Picha/Video: Madhara ya mvua iliyonyesha Dar es Salaam leo Machi 19


Goba njia 4 imedosha ukuta ukaangukia watoto 2 , na 1 kafariki.
 
Na bado siku 6 jana ilikuwa siku ya kwanza
 
Baada ya kuona hizi picha leo nakiri kuhamisha makao makuu Dodoma ni uamuzi sahihi kabisa.
Makosa ni ya serikali Dar ilitakiwa ipangwe kabla population haijawa kubwa.
 
Wacha inyeshe,
Wakazi wa mabondeni shauri yenu safari hii hakuna msaada, mmeyataka wenyewe
 
Makosa ni ya serikali dar ilitakiwa ipangwe kabla population haijawa kubwa,
Dar ni mkoa pekee unaweza kuanza kujenga bila kuwa na hati wala vibali na ukaangaliwa tu bila hatua zozote na hii mpaka leo, serikali za mitaa zipo sijui Halmashauri wewe jenga tu na hutaulizwa. Kwa sasa tumeshachelewa ni ugonjwa inabidi tuishi nao tu mpaka siku wakiweka siasa pembeni kwamba kwa yoyote aliyejenga katika njia za maji aondolewe haraka watu wasiangalieni usoni mtu kuanza kulia "mimi mjane nitawapeleka wapi watoto zangu" kila aliyejenga hana document aondoke japo najuwa halitafanyika hatuna ushujaa huo. Nategemea Dodoma hili halitatokea hasa fursa zikianza kuwa nyingi na wavamizi hutawakosa. Dodoma mpaka sasa nyumba zimepangiliwa na sheria za ujenzi zinaheshimika ila serikali isibweteke wasimamie sheria ili lisitokee tunaloliona Dar leo. Kumbuka Dar imezungukwa na bahari lakini maji hayatoki ni ajabu lakini huzuni pia ni shida ya miaka na miaka, hivi tukija kupata vimbunga sio itakuwa janga la kitaifa? Mungu atuepushe.
 
Dar imelaaniwa kutokana na mambo yanayoendelea kimboka
 
Hameni bondeni. Mfano hapo WANI HALL ni Mtoni Kabisa pamekaa wazi miaka nenda Rudi Cha ajabu Mtu kaja kuweka ukumbi na biashara zingine na anajua Wazi ni Mtoni halafu analalamika hovyo . Hameni bondeni siyo sehemu salama
 
Tatizo la Tanzania liliasisiwa na serikali kutopangilia miji na majiji kisha kuuza viwanja, ilitakiwa serikali ijimilikishe viwanja vyote
 
Tatizo la Tanzania liliasisiwa na serikali kutopangilia miji na majiji kisha kuuza viwanja, ilitakiwa serikali ijimilikishe viwanja vyote
Mbona Mbagala,Buza Gongo la Mboto hakujapangwa na hakuna Mafuriko? Endelea kufikiria vizuri tu utapata jibu.
 
Dar imeshaharibika, Magufuli aliona hapamfai
Kabisa shughuli za kiserikali na hali hii kazi haiendi ni jambo zuri sana kujenga goverment city wizara zote sehemu moja nimeona kwenye Youtube inaonekana vizuri sana na wakimaliza patapendeza sana.
 
Njia nyingi sana za maji kuelekea baharini hapo Dar es salaam zimezibwa kwa watu kujenga majumba..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…