Vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wakiongozwa na Mwenyekiti Mohammed Kawaida na Katibu Mkuu Jokate Mwegelo, wamesema wako tayari kuhakikisha wagombea wa Urais, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, wanashinda kwa kishindo.
Hii ni baada ya kufanya matembezi ya hisani katika Jiji la Dodoma kuunga mkono maamuzi ya Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Januari 18-19, 2025. K
Katibu Mkuu Jokate Mwegelo alisisitiza kuwa Vijana, akiwemo Mgombea mwenza Dkt. Emmanuel John Nchimbi, watahakikisha CCM inashika Dola. Zaidi ya Vijana 1000 walishiriki matembezi hayo.