John Gregory
JF-Expert Member
- Jul 14, 2019
- 1,137
- 2,147
Kushoto ni mchezaji kinda anayekuja kwa kasi anayechezea Kilabu cha mpira cha Simba Sc na Kulia Kabisa ni Mchezaji anayetajwa kuwa tarajio kubwa kwa kikosi hicho, Wakiwa katika picha ya pamoja na mchezaji Nyota anayekipiga katika klabu maarufu na kubwa ukanda wa mashariki ya Afrika na Afrika kiujumla,Young Africans ambayo inashiriki na kuongoza katika msimamo wa ligi kadhaa kubwa za Afrika, Fiston Kalala Mayele.
Wachezaji hao walikutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.Kwa sasa Fiston Mayele mwenye asili ya Congo DRC, Anayetajwa kuwaniwa na vilabu viwili vikubwa barani Ulaya anatarajiwa kukipiga katika timu yake ya taifa inayoshiriki katika michuano ya CHAN, The Leopards.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji hao wameshukuru na wamefurahi kupata bahati ya kukutana na nyota huyo huku wakisema ilikuwa ni ndoto zao za muda mrefu na sasa imetimia, Hivyo wanaahidi kujituma na kuongeza juhudi ili kufikia hatua kubwa iliyofikiwa na nyota huyo.
Wakati huo, Nyota huyo ameahidi kutoa ushirikiano na msaada pale itakapowezekana kwani no malengo yake ya siku nyingi kuona wachezaji wachanga wanaokuja katika soka wanafanikiwa na kutimiza ndoto zao.
REUTERS.