Picha ya Dkt. Salmin Amour na Dkt. Hussein Mwinyi inaliza

Picha ya Dkt. Salmin Amour na Dkt. Hussein Mwinyi inaliza

Aisee, kupitia haya liwe funzo kwa viongozi kuheshimu matakwa ya wananchi.God forgive him! AMINA
 
PICHA HII INAWEZA KUKUTOA MACHOZI

Dr. Salmin Amour aliyekuwa Rais wa Zanzibar alipotembelewa na Dr. Hussein Mwinyi nyumbani kwake.

Dr. Salmin kanyanyua mikono anamwelekea Allah kwa dua na dua siku zote ni kuomba kheri.

Dr. Salmin hivi sasa ni kipofu.
Haoni.

Amenyanyua mikono yake kamwelekea Allah anamuombea dua kijana wake ambae kama yeye miaka 25 iliyopita anasimama kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar katika hali ile ile ngumu na ya hatari kwa usalama wa visiwa wakati alipokuwa anamkabili Maalim Seif katika nafasi hiyo hiyo ambayo Dr. Hussein Mwinyi anaitaka na dhidi ya mtu huyo huyo na katika hali ya hatari ile ile iliyokabili Zanzibar mwaka wa 1995.

Msomaji wangu nakutaka radhi kwa sentensi ndefu nimeifanya hivyo kwa kusudi ili usivute pumzi wala kumeza mate katika msisitizo ulio ndani ya sentensi hii.

Dr. Salmin Amour alikuwa anaitwa Komando yaani mpiganaji hodari anaemudu kuzitumia silaha zote za kivita kwa ufanisi mkubwa mpiganaji ambae kifua chake kipana na mwenye misuli iliyotuna inayotisha adui.

Dr. Salmin Komando hotuba zake zilikuwa kali za kuogofya.

Leo hii sipendi kuzisikiliza hotuba za Komando kwani zinanitia simanzi kubwa wala sipendi kumwangalia popote picha zake zinapoletwa.

Hakika Kibeku alikuwa Ungo.

Wewe kijitu ukizisikia hotuba hizi lazima utatetemeka kwani wewe una nini cha kumtisha Komando?

Mabingwa wa kutengeneza filamu wa Hollywood wametengeneza movie, "David," kisa cha Mtume Daud.

Kuna kipande na Allah kakieleza kisa hiki ndani ya Qur'an pale Daud alipotoka kwenda kumkabili Jalut katika mapigano huku wote wakiangaliwa na majeshi yao.

Kisa Maarufu.

Hollywood katika ubingwa wao kipande hiki cha Daud anakwenda kupigana na Jalut wame-dramatise na kukuza kila kitu.

Kipande hiki kitakutoa machozi ukiwa utakiangalia huku unaileta ile dua ya Daud aliyokuwa anaisoma wakati anakwenda kupigana na Jalut akiwa hana silaha ila dua aliyofunzwa na Allah.

Jalut kasimama mbele yake mrefu zaidi ya futi sita na kasheheni silaha nzito na deraya mwili mzima.

Maalim Seif alimshinda Komando katika uchaguzi ule na inasemekana Maalim ameshinda kila uchaguzi yaani kawashinda marais wote wa Zanzibar aliopambananao.

Dr. Salmin anaomba dua bila shaka ya kutafuta nusra Allah avinusuru visiwa na wananchi wake na shari iliyokuwa ishasimama ikisubiri cheche ndogo kulipuka.

Dr. Salim anajua kinachomkabili Dr. Hussein Mwinyi kwani yeye kapita njia hiyo na anaijua vizuri kabisa.

Bila shaka katika dua hii yake Komando anamuomba Allah asijaalie Dr. Hussein Mwinyi akakalia kiti cha urais wa Zanzibar baada ya Wazanzibari kuuliwa.

Sote tunawajibu wa kunyonyua mikono yetu kuomba dua Allah ainusuru Zanzibar na shari ambayo tayari iko mlangoni.

Amin.View attachment 1566596
Mungu FUNDI, amempiga upofu huyu jamaa kwa kushirikiana na Mkapa kudhulumu haki ya Wazanzibari kuishi.
 
Inawezekana kabisa hata asingekua rais, Salmin angepitia hichohicho anachopitia sasa, siri ya maisha yetu anayo mwenyezi Mungu
Sisi sote ni binadamu hakuna aliyekamilika maisha yanaweza badilika muda wowote tusihukumu tusije kuhukumiwa, wala tusimpangie Mungu
Huwezi kudhulumu haki za maelfu ya Watu kuishi kisha Mwenyezi mungu akuache tu, malipo ni hapa hapa duniani. Mjulisheni na baba yenu jiwe pia.
 
Ubabe hauna mwenyewe na haulipi. Mwisho wake ni majuto. Ukomandoo huwapi sasa? Peleka salamu hizi kwa Jiwe. Kuna maisha baada ya urais.
 
Kwa kumbukumbu zangu, Maalimu Seif alikua wa kwanza kuingia kwenye siasa na hata kua na nyadhifa kubwa kubwa serikalini kuliko komandoo, binafsi nimemuona kwa mra ya kwanza Maalimu Seif April 1984 na nadhani ndio pia ilikua mara yangu ya kwanza kuiona camera ya video/TV; look at these two people now, Maalimu Seif yu buheri wa afya na komandooo afya yake ni mgogoro; kiburi hakifai, yupo Mungu mbinguni who is the controller of everything; tumuheshimu huyo. Yaani uwe una mamlaka kuliko wengine, uwe fala, uwe na pesa au fukara, kwa Mungu wote ni HALI MOJA tu
 
Kila la heri DR. Hussein,
Hakika Mungu yuko pamoja nawe,
 
Kuna watu wanaamini ukiwa rais hustahili kuumwa au kuwa mlemavu. Hii inaweza tokea hata kwa muuza viazi ambaye hajawahi hata kuiba maji ya kunywa.

Ni kipofu na sioni connection ya upofu wake na urais wake. Nchi ina maelfu ya vipovu na hawajawahi kuwa hata wenyeviti wa kugawa chakula harusini.
 
Kwa kweli wazanzibar wamepitia mengi,umefika wakati wapewe nafasi ya kuchagua viongozi na serikali wanayoitaka hiyo ni haki yao.Uchaguzi siku zote una changamoto nyingi pande zote mbili bara na visiwani,Ingawa CCM inaonekana itaendelea kutawala lakini shauku na njaa ya mabadiriko kwenye hii nchi ni wazi.Mabadiriko yatakuja sababu ni kanuni za kimaisha vitu kubadirika ila hatujui yatakujaje na lini,ingawa dalili zipo nyingi.
Mi pia naombea amani kwa nchi yote na Zanzibar kupata utawala wanaotaka na viongozi waliowachagua.
Kuna mijitu afriti inayofikiri kumuenzi baba wa taifa ni kuendelea kuwanyanyasa raia wasio na hatia Zanzibar, na tayari imeishaanza vitisho!
😱😱😱💣💥☠☠💀
 
Huwezi kudhulumu haki za maelfu ya Watu kuishi kisha Mwenyezi mungu akuache tu, malipo ni hapa hapa duniani. Mjulisheni na baba yenu jiwe pia.
Mnamlaumu bure mzee


Mimi si mjuzi wa mambo haya lakini nachoelewa unapoingia kwenye uongozi hasa wa nafasi kubwa kama urais sio suala la mimi tena bali ni suala la sisi

Unataka kuniambia unayowaza wewe au mzee Said mtu kama Shein, Karume au Salmin hayawazi?

Wakati mwingine unakuwa na dhamira fulani lakini unakutana na vigingi heavy unaishia kufanya machache unayoweza

Nasikia kuna kiongozi huko nyuma alitaka kugusa Muungano sijui ikawaje anajua mwenyewe

Maisha ni haya haya
 
Kila la heri DR. Hussein,
Hakika Mungu yuko pamoja nawe,
Mkumbusheni Dr Mwinyi, tunajua yeye ni Swala 5. Aendelee kumuogopa Mungu na akumbuke kuwa Urais unapita tu, na maisha tunapita hapa duniani. Asitamani uraisi utakao kuwa na damu na machozi ya watu wasio na hatia.
 
Kila binadam atazeeka na kunyauka hiyo ni inshu ya biological. Hata maalim kazeeka sana.
Dr Mwinyi tunamjua, ni muadilifu, mpole, huruma, mtu wa watu na mwenye hofu ya Mungu. Lakini uchaguzi ni suala la watu kuwa wanampenda nani zaidi. Asikubali kuingia mkenge wa kuwaumiza watu lwa matakwa ya kutawala
 
Leo hii sipendi kuzisikiliza hotuba za Komando kwani zinanitia simanzi kubwa wala sipendi kumwangalia popote picha zake zinapoletwa.
Shukrani kwa bandiko lako hili, Mkuu, Mohamed Said . Mimi sina mengi zaidi nilivutiwa na sentensi yako hii, hivyo nikalazimika kwenda kutafuta baadhi ya hotuba za 'Komando' huko Youtube. Na huko nimepata



Baada ya kuitazama mpaka mwisho, nimeshangazwa kwa nini, Mkuu, atiwe simanzi na hotuba kama hizi? Ukipata nafasi, unaweza kunifafanulia hili kwa ajili ya kuboresha uwelewa wangu na wa wengine wenye mtazamo kama wa kwangu.

Natanguliza shukrani.
 
Shukrani kwa bandiko lako hili, Mkuu, Mohamed Said . Mimi sina mengi zaidi nilivutiwa na sentensi yako hii, hivyo nikalazimika kwenda kutafuta baadhi ya hotuba za 'Komando' huko Youtube. Na huko nimepata



Baada ya kuitazama mpaka mwisho, nimeshangazwa kwa nini, Mkuu, atiwe simanzi na hotuba kama hizi? Ukipata nafasi, unaweza kunifafanulia hili kwa ajili ya kuboresha uwelewa wangu na wa wengine wenye mtazamo kama wa kwangu.

Natanguliza shukrani.
Tujitegemee,
Simanzi inaniingia nikimwangalia Komando akihutubia mwenye afya njema.

Leo hata ile sauti yake tuliyoizoea sote haipo.

Niliona clip yake wakati wa msiba wa Mkapa akizungumza.

Kama nisingemuona nisingejua kama huyu ni Komando.

Lakini kubwa linalonisikitisha ni kuwa alishindwa uchaguzi wa 1995.
 
Back
Top Bottom