Picha ya Dkt. Salmin Amour na Dkt. Hussein Mwinyi inaliza

Nasikia Zanzibara sasa inwekwa hadi CCTV kamera ili kuwabana vizuri.Vipi unaonaje hilo?
Zanzibar zimewekea vizingiti vya umeme ambavyo vimezikwa chini ya Ardhi,vinakuja juu kwa njia ya kuviwanja kwa umeme..

Vingiti hivyo vimewekwaa Kinazini ilipo Benki Kuu na chengine kinawekwa leo ilipo Sauti ya ( zbc)

Cha kujiuliza,Je serikali ya Mapinduzi inaogopa watu wake?
 
Tujitegemee,
Simanzi inaniingia nikimwangalia Komando akihutubia mwenye afya njema.

Leo hata ile sauti yake tuliyoizoea sote haipo.

Niliona clip yake wakati wa msiba wa Mkapa akizungumza.

Kama nisingemuona nisingejua kama huyu ni Komando.

Lakini kubwa linalonisikitisha ni kuwa alishindwa uchaguzi wa 1995.
Asante sana kwa ufafanuzi, Mkuu. Sasa nimekuelewa. Hata hivyo, maelezo yako yana mstari mwingine ambao nao umenitatiza. Ni juu ya ushindi wa urais 1995.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha The Citizen, ni kituo cha televisheni cha DTV wakati huo kilipotosha umma juu ya nani alikuwa ameshinda. Kituo hicho kilitunga matokeo yake. Kwa maelezo zaidi, Mkuu, pitia habari hiyo kwenye link hii hapa chini.

Vinginevyo, Mkuu, kama unasimamia msimamo huo nitakuomba kwa mara nyingine utupe maelezo ya kina ambayo hayatatupa mashaka juu ya ukweli wake.

LINK: Controversy surrounds 1995 Z’bar presidential poll results

Karibu.
 
PICHA HII INAWEZA KUKUTOA MACHOZI

Dr. Salmin Amour aliyekuwa Rais wa Zanzibar alipotembelewa na Dr. Hussein Mwinyi nyumbani kwake.

Dr. Salmin kanyanyua mikono anamwelekea Allah kwa dua na dua siku zote ni kuomba kheri.

Dr. Salmin hivi sasa ni kipofu.
Haoni.

Amenyanyua mikono yake kamwelekea Allah anamuombea dua kijana wake ambae kama yeye miaka 25 iliyopita anasimama kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar katika hali ile ile ngumu na ya hatari kwa usalama wa visiwa wakati alipokuwa anamkabili Maalim Seif katika nafasi hiyo hiyo ambayo Dr. Hussein Mwinyi anaitaka na dhidi ya mtu huyo huyo na katika hali ya hatari ile ile iliyokabili Zanzibar mwaka wa 1995.

Msomaji wangu nakutaka radhi kwa sentensi ndefu nimeifanya hivyo kwa kusudi ili usivute pumzi wala kumeza mate katika msisitizo ulio ndani ya sentensi hii.

Dr. Salmin Amour alikuwa anaitwa Komando yaani mpiganaji hodari anaemudu kuzitumia silaha zote za kivita kwa ufanisi mkubwa mpiganaji ambae kifua chake kipana na mwenye misuli iliyotuna inayotisha adui.

Dr. Salmin Komando hotuba zake zilikuwa kali za kuogofya.

Leo hii sipendi kuzisikiliza hotuba za Komando kwani zinanitia simanzi kubwa wala sipendi kumwangalia popote picha zake zinapoletwa.

Hakika Kibeku alikuwa Ungo.

Wewe kijitu ukizisikia hotuba hizi lazima utatetemeka kwani wewe una nini cha kumtisha Komando?

Mabingwa wa kutengeneza filamu wa Hollywood wametengeneza movie, "David," kisa cha Mtume Daud.

Kuna kipande na Allah kakieleza kisa hiki ndani ya Qur'an pale Daud alipotoka kwenda kumkabili Jalut katika mapigano huku wote wakiangaliwa na majeshi yao.

Kisa Maarufu.

Hollywood katika ubingwa wao kipande hiki cha Daud anakwenda kupigana na Jalut wame-dramatise na kukuza kila kitu.

Kipande hiki kitakutoa machozi ukiwa utakiangalia huku unaileta ile dua ya Daud aliyokuwa anaisoma wakati anakwenda kupigana na Jalut akiwa hana silaha ila dua aliyofunzwa na Allah.

Jalut kasimama mbele yake jitu la miraba minne refu zaidi ya futi sita na kasheheni silaha nzito na deraya za chuma mwili mzima.

Maalim Seif alimshinda Komando katika uchaguzi ule na inasemekana Maalim ameshinda kila uchaguzi yaani kawashinda marais wote wa Zanzibar aliopambananao.

Dr. Salmin anaomba dua bila shaka ya kutafuta nusra Allah avinusuru visiwa na wananchi wake na shari iliyokuwa ishasimama ikisubiri cheche ndogo kulipuka.

Dr. Salim anajua kinachomkabili Dr. Hussein Mwinyi kwani yeye kapita njia hiyo na anaijua vizuri kabisa.

Bila shaka katika dua hii yake Komando anamuomba Allah asijaalie Dr. Hussein Mwinyi akakalia kiti cha urais wa Zanzibar baada ya Wazanzibari kuuliwa.

Sote tunawajibu wa kunyanyua mikono yetu kuomba dua Allah ainusuru Zanzibar na shari ambayo tayari iko mlangoni.

Amin.View attachment 1566596
vifo vya wale waliouawa 2001 vinaumiza sana kumtima!
 
Inawezekana kabisa hata asingekua rais, Salmin angepitia hichohicho anachopitia sasa, siri ya maisha yetu anayo mwenyezi Mungu
Sisi sote ni binadamu hakuna aliyekamilika maisha yanaweza badilika muda wowote tusihukumu tusije kuhukumiwa, wala tusimpangie Mungu
Unapoishi na watu vizuri maisha yako hayaji kuwa sawa kama vile umeishi na watu kwa shari.
 
vifo vya wale waliouawa 2001 vinaumiza sana kumtima!
Maridhiano yalifikiwa baina ya pande zote mbili. Ikiwemo kusameheana. Kwa nini mnataka kuamsha hisia za kuumizana wakati huu!? Sidhani kama mnakusudia kuchochea vurugu Zanzibar. Nasema sidhani!
 
Ukitaka kusamehewa, usirudie kosa, inaonekana CCM Zanzibar walituchezea shere tu. Limejitokeza 2015, baada ya CCM kupora tena ushindi. Kwaio lazima tukumbushie ya 2001 maana wakosaji hawajajifunza bado.
 
Maridhiano yalifikiwa baina ya pande zote mbili. Ikiwemo kusameheana. Kwa nini mnataka kuamsha hisia za kuumizana wakati huu!? Sidhani kama mnakusudia kuchochea vurugu Zanzibar. Nasema sidhani!
Maridhiano yamefukiwa? au mliwapumbaza tu!!

Bado mnaendelea kuwaibia ushindi wao,kila kwenye kura
 
Asante sana kwa ufafanuzi, Mkuu. Sasa nimekuelewa. Hata hivyo, maelezo yako yana mstari mwingine ambao nao umenitatiza. Ni juu ya ushindi wa urais 1995.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha The Citizen, ni kituo cha televisheni cha DTV wakati huo kilipotosha umma juu ya nani alikuwa ameshinda. Kituo hicho kilitunga matokeo yake. Kwa maelezo zaidi, Mkuu, pitia habari hiyo kwenye link hii hapa chini.

Vinginevyo, Mkuu, kama unasimamia msimamo huo nitakuomba kwa mara nyingine utupe maelezo ya kina ambayo hayatatupa mashaka juu ya ukweli wake.

LINK: Controversy surrounds 1995 Z’bar presidential poll results

Karibu.
Tujitegemee,
Katika uchaguzi wa 1995 nilikuwa sehemu ya timu ya Prof. Lipumba na nilizunguka na yeye Bara na nilikuwapo Zanzibar siku ya uchaguzi.

Tume ya Uchaguzi ilianza kubabaika pale siku ya pili asubuhi matokeo yalipoonyesha kuwa Dk. Salmin Amour ameshindwa.

Katika taharuki hii Ali Ameir akaandika barua ya kukataa matokeo.
 
IMG_5768.jpg

Hapo ni maalim wakati anagombea na Komando salmin
 
PICHA HII INAWEZA KUKUTOA MACHOZI

Dr. Salmin Amour aliyekuwa Rais wa Zanzibar alipotembelewa na Dr. Hussein Mwinyi nyumbani kwake.

Dr. Salmin kanyanyua mikono anamwelekea Allah kwa dua na dua siku zote ni kuomba kheri.

Dr. Salmin hivi sasa ni kipofu.
Haoni.

Amenyanyua mikono yake kamwelekea Allah anamuombea dua kijana wake ambae kama yeye miaka 25 iliyopita anasimama kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar katika hali ile ile ngumu na ya hatari kwa usalama wa visiwa wakati alipokuwa anamkabili Maalim Seif katika nafasi hiyo hiyo ambayo Dr. Hussein Mwinyi anaitaka na dhidi ya mtu huyo huyo na katika hali ya hatari ile ile iliyokabili Zanzibar mwaka wa 1995.

Msomaji wangu nakutaka radhi kwa sentensi ndefu nimeifanya hivyo kwa kusudi ili usivute pumzi wala kumeza mate katika msisitizo ulio ndani ya sentensi hii.

Dr. Salmin Amour alikuwa anaitwa Komando yaani mpiganaji hodari anaemudu kuzitumia silaha zote za kivita kwa ufanisi mkubwa mpiganaji ambae kifua chake kipana na mwenye misuli iliyotuna inayotisha adui.

Dr. Salmin Komando hotuba zake zilikuwa kali za kuogofya.

Leo hii sipendi kuzisikiliza hotuba za Komando kwani zinanitia simanzi kubwa wala sipendi kumwangalia popote picha zake zinapoletwa.

Hakika Kibeku alikuwa Ungo.

Wewe kijitu ukizisikia hotuba hizi lazima utatetemeka kwani wewe una nini cha kumtisha Komando?

Mabingwa wa kutengeneza filamu wa Hollywood wametengeneza movie, "David," kisa cha Mtume Daud.

Kuna kipande na Allah kakieleza kisa hiki ndani ya Qur'an pale Daud alipotoka kwenda kumkabili Jalut katika mapigano huku wote wakiangaliwa na majeshi yao.

Kisa Maarufu.

Hollywood katika ubingwa wao kipande hiki cha Daud anakwenda kupigana na Jalut wame-dramatise na kukuza kila kitu.

Kipande hiki kitakutoa machozi ukiwa utakiangalia huku unaileta ile dua ya Daud aliyokuwa anaisoma wakati anakwenda kupigana na Jalut akiwa hana silaha ila dua aliyofunzwa na Allah.

Jalut kasimama mbele yake jitu la miraba minne refu zaidi ya futi sita na kasheheni silaha nzito na deraya za chuma mwili mzima.

Maalim Seif alimshinda Komando katika uchaguzi ule na inasemekana Maalim ameshinda kila uchaguzi yaani kawashinda marais wote wa Zanzibar aliopambananao.

Dr. Salmin anaomba dua bila shaka ya kutafuta nusra Allah avinusuru visiwa na wananchi wake na shari iliyokuwa ishasimama ikisubiri cheche ndogo kulipuka.

Dr. Salim anajua kinachomkabili Dr. Hussein Mwinyi kwani yeye kapita njia hiyo na anaijua vizuri kabisa.

Bila shaka katika dua hii yake Komando anamuomba Allah asijaalie Dr. Hussein Mwinyi akakalia kiti cha urais wa Zanzibar baada ya Wazanzibari kuuliwa.

Sote tunawajibu wa kunyanyua mikono yetu kuomba dua Allah ainusuru Zanzibar na shari ambayo tayari iko mlangoni.

Amin.View attachment 1566596
Mimi iiyoniliza hii hapa.

1600117540928.png
 
Mimi iiyoniliza hii hapa.

View attachment 1570102
Mkaruka,
Hakika picha hiyo ya mama mponda kokoto na mwanae kamlaza chini alale ili yeye aendelee na kazi inaliza.

Nimehamia Masaki mwishoni mwa miaka ya 1970 wakati kulikuwa na ujenzi mkubwa wa nyumba za kuishi.

Mbele ya nyumba niliyokuwa nikikaa palikuwa na uwanja mkubwa ambao hawa akina mama wakija kugonga kokote na kuuza.

Jua kali mvua kubwa wapo pale kuanzia mapema asubuhi hadi jioni wengine wakiwa na watoto wadogo migongoni.

Ukiwaangalia wanavyopigwa na jua kali la saa saba lazima utasikitika.

Picha uliyotuwekea inaliza.
 
Kuna watu wanaamini ukiwa rais hustahili kuumwa au kuwa mlemavu. Hii inaweza tokea hata kwa muuza viazi ambaye hajawahi hata kuiba maji ya kunywa.

Ni kipofu na sioni connection ya upofu wake na urais wake. Nchi ina maelfu ya vipovu na hawajawahi kuwa hata wenyeviti wa kugawa chakula harusini.
Halafu uwe mlemavu na huna hela lazima ujihisi upo jehanum... Kwangu Mimi umaskini nauona kama mojawapo ya ulemavu.
 
Inawezekana kabisa hata asingekua rais, Salmin angepitia hichohicho anachopitia sasa, siri ya maisha yetu anayo mwenyezi Mungu
Sisi sote ni binadamu hakuna aliyekamilika maisha yanaweza badilika muda wowote tusihukumu tusije kuhukumiwa, wala tusimpangie Mungu
Inawezekana hakika, lakini mantiki hapa ni kibri akivaacho mwanadamu apatapo siha mfano wa huyo bwana, kwamba hudhani atabaki hivyo kilele Sasa si lolote si chochote
 
Mkaruka,
Hakika picha hiyo ya mama mponda kokoto na mwanae kamlaza chini alale ili yeye aendelee na kazi inaliza.

Nimehamia Masaki mwishoni mwa miaka ya 1970 wakati kulikuwa na ujenzi mkubwa wa nyumba za kuishi.

Mbele ya nyumba niliyokuwa nikikaa palikuwa na uwanja mkubwa ambao hawa akina mama wakija kugonga kokote na kuuza.

Jua kali mvua kubwa wapo pale kuanzia mapema asubuhi hadi jioni wengine wakiwa na watoto wadogo migongoni.

Ukiwaangalia wanavyopigwa na jua kali la saa saba lazima utasikitika.

Picha uliyotuwekea inaliza.
Kipindi hicho Ndio unaanza maisha maana mwaka 1980 Ndio ulikuwa na miaka 28 yaani kabwana kadogo kabisa, moh huwa unanifurahisha unavyusimulia matukio na watu waliokuzidi umri asiefahamu umri wako huenda akadhani wewe ni umri wakina Bomani au Butiku Kumbe hata 70 hujafika. Hongera
 
Kuna watu wanaamini ukiwa rais hustahili kuumwa au kuwa mlemavu. Hii inaweza tokea hata kwa muuza viazi ambaye hajawahi hata kuiba maji ya kunywa.

Ni kipofu na sioni connection ya upofu wake na urais wake. Nchi ina maelfu ya vipovu na hawajawahi kuwa hata wenyeviti wa kugawa chakula harusini.
Connection ipo, Ndio maana tunaambiwa kufanya mema tukiwa na afya, muhali mtu atakae kuja dhoofu baada ya siha iliyombidiisha kufanya mema si sawa na alighulika na afya njema kwa kujivika kibri, Salmin amour angelikuwa hivyo umri wake wote sidhani kama angelikuwa na jeuri ile ya ukomandoo
 
Back
Top Bottom