- Source #1
- View Source #1
MADAI
Kumekuwepo na picha inayozunguka mtandaoni ikimuonesha mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe akizungumza na Rais Samia huku mandhari ya nyuma ya picha hiyo kukiwa na chombo chenye asali ndani yake.
Ukweli wa picha hii upoje?

Picha inayodaiwa kuwa na chombo chenye asali
Picha halisi iliyotolewa na Ikulu
Picha halisi iliyotolewa na Ikulu
- Tunachokijua
- Picha ya tukio hili ilichukuliwa Disemba 31, 2022, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndugu. Abdulrahman Kinana wakati akipokea taarifa ya Maendeleo ya mazungumzo ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kwa kutazama picha ya pili iliyowekwa kwenye mitandao rasmi ya kijamii ya Ikulu, hakuna chombo chenye asali kama mtoa mada alivyoelezea hivyo madai haya siyo ya kweli.