Picha ya Hemed Mashaka Mdose na Mwalimu Nyerere Kura Tatu Tabora 1958

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
PICHA YA BABA WA TAIFA YA MKUTANO WA KURA TATU 1958 KUTOKA MAKTABA YA MZEE HEMEDI MASHAKA MDOSE TABORA

John Iliffe alipata kusema katika miaka ya mwishoni 1960 wakati akiwa mwalimu wa historia University of East Africa, Dar es Salaam kuwa historia ya TANU iko katika mikono ya watu binafsi.

Mimi nimeyakubali maneno haya zamani sana kwani nimeona nyaraka nyingi za historia ya uhuru wa Tanganyika pamoja na picha kwa watu ambao wala huwezi kuwadhania kuwa walikuwa mstari wa mbele na bega kwa bega na Mwalimu Nyerere ndani ya TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Watu hawa historia zao zimefutika na hakuna anaewajua.

Wengi katika watu hawa wametangulia mbele ya haki miaka mingi nyuma.

Leo nimepigiwa simu na rafiki yangu Joseph Mayuni kutoka Tabora akanieleza kuwa hapo alipo yuko na mzee ambae aliniambia kuwa ana historia yote ya TANU Tabora anaomba nizungumzenae.

Huyu mzee nimebahatika sana kuzungumza na yeye na ana umri wa miaka 89.

Jina lake ni Hemed Mashaka Mdose mwenyeji wa Tabora.
Picha yake ipo hapo hapo chini inamwonyesha kama alivyo hivi sasa.

Haraka tukaingia katika maongezi na nikamfahamisha kuwa asili ya wazee wangu ni mji huo na nikamfahamisha jina la babu yangu ''Baba Popo'' kama alivyokuwa akifahamika.

Mzee Hemed jibu lake lilikuwa, ''Wa Isevya,'' akiwa na maana ya kuniambia kuwa babu yangu alikuwa akiishi Isevya.

''Wewe mtoto wa nani?''
''Said.''

Mzee Hemed akaniongezea, ''Said Popo.''
Akionyesha kuwa alikuwa akimjua baba yangu vizuri sana.

Mzee Hemed maisha yake yote alikuwa mshoni fundi cherehani akifanya shughuli zake Gongoni Uhindini na alikuwa mmoja wa vijana waliojiunga na TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wakati huo alikuwa kijana mdogo wa miaka 20.
Picha inasema maneno 1000.

Mzee Hemed ametutunuku na picha yake akiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa mwezi Januari, 1958 wakati wa mkutano wa Kura Tatu.

Katika picha hiyo hapo chini wa kwanza lakini haonekani ila mkono wake tu ni Haruna Ibrahim Lipumba (baba yake Prof. Ibrahim Haruna Lipumba), Kassim Said Mwinyigoa, Julius Nyerere, Hemed Mashaka Mdose na Ramadhani Mdoe Mdose.

Ramadhani Mdoe Mdose ni baba yake mdogo Mzee Hemed Mdose anaonekana amevaa nembo katika shati lake iliyoandikwa ''Bantu Group.''

Bantu Group ilianza Dar es Salaam likiwa ni kundi la vijana wana TANU waliokuwa wahamasishaji na walinzi wa viongozi wa TANU.

Picha hii inastahili kutundikwa katika ofisi za CCM Dodoma na Dar es Salaam.

Picha hii imebeba ujumbe mkubwa sana.

343611020_3492096961035256_4054381697134320977_n.jpg
343480059_625236965730044_5193892374926615826_n.jpg
 
PICHA YA BABA WA TAIFA YA MKUTANO WA KURA TATU 1958 KUTOKA MAKTABA YA MZEE HEMEDI MASHAKA MDOSE TABORA

John Iliffe alkipata kusema katika miaka ya mwishoni 1960 wakati akiwa mwalimu wa historia University of East Africa, Dar es Salaam kuwa historia ya TANU iko katika mikono ya watu binafsi.

Mimi nimeyakubali maneno haya zamani sana kwani nimeona nyaraka nyingi za historia ya uhuru wa Tanganyika pamoja na picha kwa watu ambao wala huwezi kuwadhania kuwa walikuwa mstari wa mbele na bega kwa bega na Mwalimu Nyerere ndani ya TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Watu hawa historia zao zimefutika na hakuna anaewajua.

Wengi katika watu hawa wametangulia mbele ya haki miaka mingi nyuma.

Leo nimepigiwa simu na rafiki yangu Joseph Mayuni kutoka Tabora akanieleza kuwa hapo alipo yuko na mzee ambae aliniambia kuwa ana historia yote ya TANU Tabora anaomba nizungumzenae.

Huyu mzee nimebahatika sana kuzungumza na yeye na ana umri wa miaka 89.

Jina lake ni Hemed Mashaka Mdose mwenyeji wa Tabora.
Picha yake ipo hapo hapo chini inamwonyesha kama alivyo hivi sasa.

Haraka tukaingia katika maongezi na nikamfahamisha kuwa asili ya wazee wangu ni mji huo na nikamfahamisha jina la babu yangu ''Baba Popo'' kama alivyokuwa akifahamika.

Mzee Hemed jibu lake lilikuwa, ''Wa Isevya,'' akiwa na maana ya kuniambia kuwa babu yangu alikuwa akiishi Isevya.

''Wewe mtoto wa nani?''
''Said.''

Mzee Hemed akaniongezea, ''Said Popo.''
Akionyesha kuwa alikuwa akimjua baba yangu vizuri sana.

Mzee Hemed maisha yake yote alikuwa mshoni fundi cherehani akifanya shughuli zake Gongoni Uhindini na alikuwa mmoja wa vijana waliojiunga na TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wakati huo alikuwa kijana mdogo wa miaka 20.
Picha inasema maneno 1000.

Mzee Hemed ametutunuku na picha yake akiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa mwezi Januari, 1958 wakati wa mkutano wa Kura Tatu.

Katika picha hiyo hapo chini wa kwanza lakini haonekani ila mkono wake tu ni Haruna Ibrahim Lipumba (baba yake Prof. Ibrahim Haruna Lipumba), Kassim Said Mwinyigoa, Julius Nyerere, Hemed Mashaka Mdose na Ramadhani Mdoe Mdose.

Ramadhani Mdoe Mdose ni baba yake mdogo Mzee Hemed Mdose anaonekana amevaa nembo katika shati lake iliyoandikwa ''Bantu Group.''

Bantu Group ilianza Dar es Salaam likiwa ni kundi la vijana wana TANU waliokuwa wahamasishaji na walinzi wa viongozi wa TANU.

Picha hii inastahili kutundikwa katika ofisi za CCM Dodoma na Dar es Salaam.

Picha hii imebeba ujumbe mkubwa sana.

343611020_3492096961035256_4054381697134320977_n.jpg
343480059_625236965730044_5193892374926615826_n.jpg
Maalim nakushukuru kwa nondo muhimu kama hii Swali langu dogo,ni kwa nini picha hiyo itundikwe ofisi ya ccm na siyo cuf,act wala.chadema?
 
Mkuu

Mkuu kwani cud,act na chadema wana ugomvi na TANU.
Bali...
Sielewi hili la ugomvi wa vyama ulivyotaja limeingiaje katika historia ya TANU.

Picha niliyoweka hapo ni ya TANU katika mikutano wa Kura TATU Tabora mwaka wa 1958.

CCM ndiyo warithi wa chama cha TANU.

Hii ndiyo sababu ya CCM kuhusika na historia ya Kura Tatu.
 
mkuu,tatizo langu Mimi ni kwamba ,TANU ni ya watanzania wote na si ccm peke yao.Mambo yote ya TANu ya faa yawekwe ofisi za serikali badala ya ccm.
 
Bali...
Sielewi hili la ugomvi wa vyama ulivyotaja limeingiaje katika historia ya TANU.

Picha niliyoweka hapo ni ya TANU katika mikutano wa Kura TATU Tabora mwaka wa 1958.

CCM ndiyo warithi wa chama cha TANU.

Hii ndiyo sababu ya CCM kuhusika na historia ya Kura Tatu.
mkuu,tatizo langu Mimi ni kwamba ,TANU ni ya watnzania wote na si ccm peke yao.Mambo yote ya TANu ya fa a yawekwe of is za serikali badala ya ccm
 
Back
Top Bottom