- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kuna picha inasambaa ikimuonesha Messi akiwa anamuogesha Yamal wakati Yamal akiwa mtoto. Naomba kufahamu ukweli wa ile picha na ilikuwaje Messi akakatuna na Wazazi wa Yamal enzi hizo.
- Tunachokijua
- Lamine Yamal Nasraoui Ebana ni mchezaji wa timu ya taifa ya Uhispania aliyezaliwa Julai 13, 2007. Yamal alijiunga na klabu ya Barcelona akiwa na umri wa miaka 7 kutoka klabu ya mtaani kwake CF La Torreta.
Baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya EURO 2024 inayoendelea Ujerumani, Lamine Yamal amezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ubora wake na jinsi anavyoweza kutawala soka miaka michache ijayo.
Picha za Yamal akiwa na Lionel Messi
Usiku wa Julai 9, 2024 zilianza kusambaa picha mbili za Lamine Yamal, moja akiwa amebebwa na Lionel Messi na nyingine akiwa amekaa kwenye beseni akiogeshwa na mchezaji huyo nguli wa soka duniani.
Aidha, mmojawapo wa watumiaji wa Mtandao wa X (Ayubu Madenge), Julai 10, 2024 alichapisha ujumbe wenye ufafanuzi wa mojawapo ya picha hizo ikisema "Barcelona ilikuwa na Utaratibu wa kupiga picha na watoto kwa ajili ya Calender ya UNICEF. Mwaka 2007, Messi akiwa na Miaka 20 akapangiwa kupiga picha na mtoto mchanga wa Miezi 4 ambaye ni Lamine Yamal. Wakati huo hakuna alijua kuwa Yamal angekuja kuwa mchezaji hodari namna hii"
Picha hizi ni halisi?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa picha hizi ni halisi, zilichukuliwa miezi michache baada ya kuzaliwa kwa Yamal mwaka 2007, wakati huo Messi akiwa na umri wa miaka 20.
Kwa mujibu wa mpiga picha aliyeshiriki kwenye tukio hilo, Joan Monfort, nguli wa soka duniani Lionel Messi alipiga picha na watoto wa familia kadhaa kwenye mradi wa hisani uliokuwa unasimamiwa na Shirila la UNICEF. Anafafanua kuwa zoezi hilo halikuwa rahisi maana Messi ni mtu siyezungumza sana, pia ana aibu.
Aidha, Julai 5, 2024, baba yake Lamine kwenye ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Instagram alichapisha picha ikimuonesha Lamine akiwa kwenye beseni la bluu huku mama yake pamoja na Messi wakiwa wamemshika wakimuogesha. Picha hii iliambatana na maneno yanayosema 'The beginning of two legends'
Chanzo: InstagramHoja nyingine inayothibitisha uhalali wa picha hii ni kupitia chapisho la Lamine Yamal aliloweka kwenye akaunti yake rasmi ya Mtandao wa X Julai 10, 2024, likiwa na picha akiwa amebebwa na Messi ikiambatana na maneno 'Reborn'.