Picha ya mmiliki wa home shopping center

Picha ya mmiliki wa home shopping center

Du ni kweli huyu jamaa alikuwa na hasira sana kubeba kiasi kikubwa vivyo cha Tindikali na MUNGU amlinde asikamatwe, kwani ametulipia na sisi ndugu zetu waliouawa na eti kuwalipwa machungu.

Moja ya matukio hayo ni kumpiga risasi mfanyakazi wake mwaka 2005 wakati akishusha bidhaa za kuuza dukani kutoka katika gari lake, kumpiga risasi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Vingunguti, Deo Vicent Agosti 15, 2006 saa 1:00 usiku Mtaa wa Msimbazi na Swahili Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Mfanyakazi wake alimpiga baada ya kumbishia Said kwamba hawezi kumpiga risasi kwa sababu anajua sheria za nchi haziruhusu kufanya hivyo. Alimpiga kuonyesha kwamba yeye yupo juu ya sheria za nchi. Kesi hiyo nayo aliimaliza kimya kimya kwa kumpa hela mfanyakazi huyo na ndugu zake na polisi.

Mtoto Vicent yeye baada ya kupigwa risasi aliliripoti Polisi na baadaye alilazwa katika Wodi namba 17 Moi kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Alipigwa risasi ya mguuni wakati akipita karibu na duka la Said baada ya mashabiki wa Simba waliokuwa wakisherekea ushindi wa timu yao kupita katika eneo hilo.
Hata hivyo, alimaliza kesi hiyo nje ya mahakamani kwa kuwapa hela wazazi wa mtoto huyo.

Every bad thing you do comes back to you, killing ain't fair but somebody got to do it - Tupac Shakur
 
.....pole sana Said...Mungu akusaidie upone upesi tujue ukweli wa hili jambo.........
 
What goes around comes around. Wabongo wamechoka kupeleka kesi polisi ni umafia tu... if you do me, i do you.
 
Ila kusema kweli nchi hii hatuna serikali. Hivi serikali inashindwa kudeal na wahalifu kama hawa? Hivi kupambana na CDM wanaoandamana na kufanya shughuli zao kwa amani ndio kazi ya serikali na vyombo vya usalama?
Hivi Rais Kikwete hajui hawa wahalifu, huu si ndio mtandao wake na wafadhili wake? Ndio maana wanapambana na CDM na kuzushia udini na ukabila vyama vinavyokuwa tishio kwao kwasabau wanaogopa kuibuliwa maovu yao? Said, Rostam, Manji? Hutakuta Ridhiwani anahusika na biashara zao hizo? Oh my God. Ndio maana JK majina ya wauza madawa ya kulevya anajua na anatamka hadharani lakini hatangazi waliofikishw mahakamani. Hivi Tukirudi kwenye nyara za serikali hapo si tunamkutapo yule katibu jangili. Maweeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!! Tumekweisha!
Pole kwa kumwagiwa tindikali ila kama kweli we ni muovu kiasi hicho Mungu akusamehe pia ubadilike.
 
huyo alistahili akirudi akaendelea na zake watammaliza kabisa
 
Hii inatisha! Hivi mtu unawezaje kumfanyia mwanadamu mwenzako kitendo kama hiki?

mbona yeye aliwafanyia wenzake hivyohivyo. Si vizuri kumwambea mtu mabaya wanajamvi mtanisamehe ila wacha akome
 
mbona yeye aliwafanyia wenzake hivyohivyo. Si vizuri kumwambea mtu mabaya wanajamvi mtanisamehe ila wacha akome

Bakeza kama ulikuwa akilini mwangu vile.. muosha huoshwa! duu?? yaani yaliyo orodheshwa yote kama aliyafanya kweli he really deserve it!
 
Hii inatisha! Hivi mtu unawezaje kumfanyia mwanadamu mwenzako kitendo kama hiki?
Na eana tuhuma za kuwaingilia kinyume na maumbile wafanyabiashara wapinzani wenzake kama ni kweli
 
Back
Top Bottom