Picha ya mwili wa Alphonce Mawazo huwa inanifanya niwaone waliochagua kuwa wapagani wako sahihi kujitenga na unafiki wa sisi tunaojidai kumjua Mungu

Picha ya mwili wa Alphonce Mawazo huwa inanifanya niwaone waliochagua kuwa wapagani wako sahihi kujitenga na unafiki wa sisi tunaojidai kumjua Mungu

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Leo ikiwa ni siku ambayo kamanda Mawazo aliuwawa mwaka 2015,picha za mwili wake ukiwa umevujaa dama zimesambaa huko twitter kama kumbukumbu ya tukio hilo la kinyama.

Waliotenda unyama ule sijui kama waliowahi kamatwa, ila kibaya ni watu wa chama fulani kutojali unyama huu na kutumia nguvu kubwa kubeza matukio ya aina hii.

Binafs huwa nafika mahali na kuwakubali waliachagua kuwa wapagani au wale waliochagua kuabudu sanamu na Mungu mingine.

Hivi kweli wewe kama una dini na kila siku ya ibada tunaenda kuabudu, unaweza kweli kuona ile picha na ukaipuuza na ukaendelea kuwa shabiki wa watu waliohusika na mauji ya aina hii kisa tu kujipendekeza ili ukumbuke au ulinde ugali wako?

Hakika bora wapagani kuliko sisi tunaojidai kumjua Mungu lakini roho zetu ni za kinyama kwa kiwango cha juu mno!
 
Chadema mmewatelekeza wanachama wenu magerezani wanakosa hata mawakili idara yenu ya sheria inakwama sana.
 
Hyo picha iko wap mkuu...mbna unatutisha usku usku huu
 
Vipi picha za Chacha Wangwe alipotaka uenyekiti wa Chadema?
 
Back
Top Bottom