SI KWELI Picha ya raia wa Zimbambwe baada ya kurudi akitokea Afrika Kusin tangu 2009

SI KWELI Picha ya raia wa Zimbambwe baada ya kurudi akitokea Afrika Kusin tangu 2009

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kumekuwepo Picha inayosambazwa kwenye mitandao ya Facebook, Instagram na X (zamani Twitter) kumuonesha mwanaume wa Zimbabwe aliyekwenda Afrika Kusini mwaka 2009 na kurejea nyumbani baada ya miaka 16 kufuatia mashambulizi dhidi ya wahamiaji (xenophobic attacks), ambapo amekuta nyumba ya familia ikiwa imeharibika na wazazi wake wakiwa wamefariki.

Katika kufuatilia zaidi kuhusu picha hiyo kwa kutumia nyenzo za kigijital imebanika kuwa Hakuna taarifa kutoka vyombo vya habari vya kuaminika au rekodi zinazothibitisha tukio hilo au kumtambulisha mtu huyo.

Sambamba na hivyo kumeendelea kuwepo na picha nyingi zenye mfanano na hiyo zikichapishwa hapa, hapa, hapa, hapa

Ingawa kumekuwa na visa vya wahamiaji wa Zimbabwe kurejea nyumbani kutokana na mashambulizi dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini, simulizi linaloambatana na picha hiyo halijathibitishwa.

Aidha, picha hiyo imekuwa ikisambazwa wakati ambapo makundi ya wanaharakati kama March & March yanaendesha kampeni zinazolenga kuwataka wahamiaji wasio na nyaraka kuondoka nchini Afrika Kusini, hali iliyochochea hofu na matukio ya vurugu dhidi ya wageni.

Hadi sasa taifa la zimbvambwe limefanikiwa kuwaondoa raian wao zaidi ya 660 kutokana na makundi ya wana harakati wanao dai raia wasio na vibali kuondoka nchini afrika kusin kama ilivyo ripotiwa hapa

Katika ufutiliaji mwingine kwa mbinu za kidigital imethibitika kuwa picha hiyo imetengezwa kwa kutumia teknlojia ya akili unde kwa lengo la kuhusanisha kile ambacho kinatokea na kuendelea nchini afrika kusini.
ZIMBAMBWE.jpg
 
Back
Top Bottom