Picha ya Rais vs Rais wa Picha

Picha ya Rais vs Rais wa Picha

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Nimekaa nikatafakari nikajiuliza hivi aliyekamatwa na kuwekwa korokoroni kwa sababu ya kuchoma picha ya Rais ameonewa? Je, emetendewa haki?

Kisha nikajiuliza je, Rais kwa kuchomwa picha yake ameonewa? Ametendewa haki?

Kisha nikajiuliza je, kitendo cha kuchoma picha ya Rais ni sawa na kumchoma Rais? Ama siye tunaye Rais wa picha?

Kama tunaye Rais wa picha basi kuchoma picha ya Rais ni sawa na kumchoma Rais kwa sababu ni Rais wa picha.

Kwa ufupi sasa mahakama na mfumo wetu wa haki umethibitsha beyond reasonable doubts kwamba kuchoma picha ya Rais ni sawa na kumchoma moto rais.sawa kwa sisi ambao tunafikra kubwa sasa hivi tukikuta gazeti laina picha ya Rais tunajua nini cha kufanya maana tunajua huku alipo ataungua tu ndio maana inabidi sasa watu wapigwe marufuku kuchoma picha yake.

Kwa wanasheria mlioko huku mtusaidie tu kwamba ilikuwaje kuchoma picha ya Rais ikawa jinai tena ya kufungwa jela
 
Hivi yule kijana alichoma moto picha ya aina gani ya Rais?

Maana kwa akili yangu ya huku kijijini; picha ya Rais ni ile iliyotundukiwa kwenye majengo ya serikali na taasisi nyingine! Yaani ni ile picha rasmi katika hayo majengo! Na ikitokea nikaiondoa sehemu ilipotundikwa, na kwenda kuichoma moto; hapo nitakuwa nimefanya kosa la jinai.

Ila siyo hii picha ya kudowload, na kuamua kuichoma moto! Sidhani kama nitakuwa nimefanya kosa la kusababisha kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa.
 
Hivi picha zote za Mkuu zilizotundikwa kwenye milingoti ya umeme nchi nzima huwa zinapelekwa wapi baada ya kwisha matumizi yake? Je zinahifadhiwa kwenye makumbusho ya taifa? Je zinazikwa kwa heshima zote au zinachomwa pia? 😳 :AYOOO:🤔
 
Anatafutwa mkandarasi wa kuzichoma
 
Nimekaa nikatafakari nikajiuliza hivi aliyekamatwa na kuwekwa korokoroni kwa sababu ya kuchoma picha ya Rais ameonewa? Je, emetendewa haki?

Kisha nikajiuliza je, Rais kwa kuchomwa picha yake ameonewa? Ametendewa haki?

Kisha nikajiuliza je, kitendo cha kuchoma picha ya Rais ni sawa na kumchoma Rais? Ama siye tunaye Rais wa picha?

Kama tunaye Rais wa picha basi kuchoma picha ya Rais ni sawa na kumchoma Rais kwa sababu ni Rais wa picha.

Kwa ufupi sasa mahakama na mfumo wetu wa haki umethibitsha beyond reasonable doubts kwamba kuchoma picha ya Rais ni sawa na kumchoma moto rais.sawa kwa sisi ambao tunafikra kubwa sasa hivi tukikuta gazeti laina picha ya Rais tunajua nini cha kufanya maana tunajua huku alipo ataungua tu ndio maana inabidi sasa watu wapigwe marufuku kuchoma picha yake.

Kwa wanasheria mlioko huku mtusaidie tu kwamba ilikuwaje kuchoma picha ya Rais ikawa jinai tena ya kufungwa jela
Kwani mapicha yote ya Rais yakibandikwa mitaani na kutolewa huwa yanatunzwa kwa ajili ya vizazi vijavyo?
 
Hivi picha zote za Mkuu zilizotundikwa kwenye milingoti ya umeme nchi nzima huwa zinapelekwa wapi baada ya kwisha matumizi yake? Je zinahifadhiwa kwenye makumbusho ya taifa? Je zinazikwa kwa heshima zote au zinachomwa pia? 😳 :AYOOO:🤔
Mkuu umemaliza kila kitu🤣, hii nchi ngumu sana
 
Kwa wanasheria mlioko huku mtusaidie tu kwamba ilikuwaje kuchoma picha ya Rais ikawa jinai tena ya kufungwa jela
Bado tupo level ya chini kabisa ya viumbe, bado tuna'evolve'; tutakapofikia hatua ya juu ya viumbe nasi tutaelewa kwamba rais ni mtu tu, kama watu wengine. Na kwa kuwa ni kiongozi anao waongoza watakuwa na hisia mbalimbali juu yake. Wengine watatamani kabisa hata kumla mzima mzima wakipata nafasi ya kumfikia karibu. Sasa hawa kwa vile hawawezi kumfikia karibu, hasira zao zinapitia kwenye hayo ya kumchoma kwenye picha na anakufa kabisa, anapotea kwenye maisha yao!
Ni upumbavu kufunga watu jela kwa kumaliza hasira zao kwenye picha ya mtu wasiye mthamini maishani mwao.
 
Ila siyo hii picha ya kudowload, na kuamua kuichoma moto! Sidhani kama nitakuwa nimefanya kosa la kusababisha kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa.
Hapana.
Ichukue hiyo picha ya ku-'down-load'; halafu itisha kikundi cha watu na ku-download' mahasira yako kwenye picha hiyo na kuichoma moto. Ni lazima pawepo na tendo la aina hiyo.
Binafsi bado sikubaliani ni huo ujinga wa kushtaki watu kwa mambo ya kipuuzi kama hilo.
Hili la rais naliona kuwa tofauti na tendo la kuchoma bendera ya nchi kwa mfano.
 
Hivi nikinunua gazeti lenye picha ya rais, natakiwa nilifanyeje hilo gazeti baada ya kulisoma?
Usiende nalo mtaani kwenu na kuwaonyesha majirani hiyo picha, na kisha kuchoma gazeti!
Mi nadadisi tu, sijui jibu.

Na hata ukienda nalo sokoni kwa muuza nyama, chunga sana, usilitumie gazeti kufungashia nyama yako.
Lakini inawezekana, ukienda mafichoni, kama kule palipo na tundu kwenye shimo refu; ukalitumia kumaliza kazi yako, hapo ni ruhusa!

La muhimu hapa, pasiwepo na 'chawa' karibu nawe unapolitumia hilo gazeti.
 
Picha yako
Sasa picha yangu inaingiaje hapo? Umesema picha ya Rais na yeye mwenyewe ni nembo ya taifa, nikakuuliza picha Gani? Nilitarajia uniambie picha inayotumika rasmi kwenye maofisi au picha yoyote ya Rais iwe ya kuchora au kutengeneza Kwa namna yeyote ile.
 
Nmesema picha ya rais afu unauliza picha ya nani tena? Kwan picha ya rais uliyoichora getto kwako anaonekana nani kwenye hy picha!
 
Back
Top Bottom