Picha ya Rais vs Rais wa Picha

Picha ya Rais vs Rais wa Picha

Hivi picha zote za Mkuu zilizotundikwa kwenye milingoti ya umeme nchi nzima huwa zinapelekwa wapi baada ya kwisha matumizi yake? Je zinahifadhiwa kwenye makumbusho ya taifa? Je zinazikwa kwa heshima zote au zinachomwa pia? 😳 :AYOOO:🤔
Kiberiti cha TINGA TINGA kinahusika
 
kama twiga vile?
Sasa kuna ubaya gani kuchoma picha ya twiga?
Hufungwi wala hutozwi Million 5 hata ukichoma Misimbazi yako hufungwi utaletewa zengwe tu kwamba km unazo nyingi na Sisi tugawie kidogo usizichome moto
 
Hapo muhimu ni kuhakikisha kiongozi wetu havurugwi kihisia!!
 
Hivi yule kijana alichoma moto picha ya aina gani ya Rais?

Maana kwa akili yangu ya huku kijijini; picha ya Rais ni ile iliyotundukiwa kwenye majengo ya serikali na taasisi nyingine! Yaani ni ile picha rasmi katika hayo majengo! Na ikitokea nikaiondoa sehemu ilipotundikwa, na kwenda kuichoma moto; hapo nitakuwa nimefanya kosa la jinai.

Ila siyo hii picha ya kudowload, na kuamua kuichoma moto! Sidhani kama nitakuwa nimefanya kosa la kusababisha kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa.
Dogo ni mchoraji! Bila shaka picha (sanamu ile) aliichora mwenyewe. Tena kwa gharama. Lakini kadri muda ulivyozidi kwenda hakuona sababu za kuichora!
Kingine cha ajabu... Mbona kesi ile kesi iliendeshwa kwa haraka/dharura kiasi kile?
 
Kitendo cha kuchoma picha ya Rais ni kibaya sana na kinaweza kuleta mtafaruku na uvunjifu wa amani kwenye jamiii. Kitendo hiki kinaweza kuleta amsha amsha mbaya kabisa, tukabonda mawe misafara ya viongozi nao wakalipa kwa kumwaga jeshi na FFU, marungu, viwiko na mateke.

Ila ukisikiliza vizuri video kijana hataji popote jina la Bimkubwa Vasco Da Gama, anasema tu kosa la Mama kutokemea ushoga na anamualika Mazeri amtembelee kule bush anapopatikana!!

Halafu, ukiangalia vizuri video inaonesha pale alipo kijana kuna moto chini unawaka ila chini hatuoneshwi kisha kijana anamiminia picha ya Bimkubwa kimiminika hatujui ni mafuta au maji kisha anaitupa chini picha ila hatuoneshwi picha inapotua chini na hata inapoungua moto.

yani inaonesha wazi kijana ana bush lawyers!!
 
Dogo ni mchoraji! Bila shaka picha (sanamu ile) aliichora mwenyewe. Tena kwa gharama. Lakini kadri muda ulivyozidi kwenda hakuona sababu za kuichora!
Kingine cha ajabu... Mbona kesi ile kesi iliendeshwa kwa haraka/dharura kiasi kile?
Hiyo video umeiona?
 
Kashtakiwa sababu ya hawa watu chini...
IMG_20240706_031823.jpg
 
... kuna (1) kuchoma picha ya mtu na (2) kuchoma picha ya mtu hadharani kwa lengo la kumdhalilisha! ... hivi ni vitu viwili tofauti!
Inapokuwa namba (2) hapo juu imefanywa dhidi ya rais wa jamhuri ya muungano kuna vifungu vya sheria vinavyoweza kumlinda au kumuingiza hatiani muhusika!
TUACHE VYOMBO VYA SHERIA VIFANYE KAZI YAKE ILI HAKI ITENDEKE!
NB: KAMA MUHUSIKA ATATHIBITIKA KUWA ANA MAGONJWA YA AKILI BASI TIBA ITAHUSIKA!
 
Bado tupo level ya chini kabisa ya viumbe, bado tuna'evolve'; tutakapofikia hatua ya juu ya viumbe nasi tutaelewa kwamba rais ni mtu tu, kama watu wengine. Na kwa kuwa ni kiongozi anao waongoza watakuwa na hisia mbalimbali juu yake. Wengine watatamani kabisa hata kumla mzima mzima wakipata nafasi ya kumfikia karibu. Sasa hawa kwa vile hawawezi kumfikia karibu, hasira zao zinapitia kwenye hayo ya kumchoma kwenye picha na anakufa kabisa, anapotea kwenye maisha yao!
Ni upumbavu kufunga watu jela kwa kumaliza hasira zao kwenye picha ya mtu wasiye mthamini maishani mwao.
... we can't be as lawless as the animals we evolved from and call ourselves humans!
😅
 
Kwahiyo yale magazeti tunayofungiwaga mihogo na wengine kuchambia huwa tunachambia nembo ya nchi?
fanya hvy hadharani utajua vzr, mana hata huyo jamaa angechoma ile picha akiwa getto kwake asingepata shida.
 
Back
Top Bottom