Picha ya siku: Kinachoendelea Afrika Kusini

Picha ya siku: Kinachoendelea Afrika Kusini

Kinachoendelea Afrika kusini ni baada ya kuwepo kwa:

1.Uongozi mbovu katika nchi,yaani kuwa na Taifa ambalo uongozi umefeli kudeliver leadership.

2.Tofauti ya kipato na maisha kati ya Tajiri na masikini kuwa kubwa sana.

3.Ukosefu wa ajiri uliopitiliza.

4.Watu kuwa na chuki pamoja na vinyongo moyoni pasipo kujua hata adui yao ni nani.

5.Mgawanyo usio sahihi wa keki ya Taifa.Wachache ndiyo wanaofaidi cake hiyo.

6.Kukosekana kwa utawala wa sheria wa walio wengi,yaani sheria zimetungwa na wahuni wachache kwa manufaa yao.

7.Watu kuwa na matatizo ya akili yaliyochangiwa na umasikini wa kutupwa.

8.Taifa kuwa na watu wengi ambao hawana cha kupoteza kwa hiyo wapo tayari kwa lolote.

9.Watu kujua ukweli kuwa wananyonywa na system za uongozi pamoja na system za kugawa utajiri

10.Dalili za awali za failure state.

View attachment 1851524
Harafu Kuna watu wanadai,hao wanaofanya fujo,wanasukumwa na mapenzi waliyonayo kwa Mtu wa kabila lao Zuma
 
Back
Top Bottom