PostGE2025 Picha ya Siku: Ridhiwani Kikwete pamoja na Jesca Magufuli katika utulivu mkubwa Bungeni

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,476
Reaction score
26,173
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio Picha ya Siku kutoka Bungeni ikiwaonyesha Viongozi wetu na watumishi wetu Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete pamoja na Mheshimiwa Jesca Magufuli vijana wetu wachapakazi,wacha Mungu,wapole wanyenyekevu,wasio na Makuu wala majivuno wala kiburi wala dharau kwa mtu.

Vijana ambao wamelelewa katika maadili mazuri na yenye kupendeza na kuigwa na kila mtu. Maadili ambayo huwezi hata kujua au kutambua kama ni watoto ambao Baba zao waliwahi kuongoza Taifa letu kama Ma Rais. Vijana ambao huwezi kuona au kukuta wakijikweza au kutumia Majina ya Baba zao kuringa au kujivunia au kumuonea mtu au kuvunja sheria.

Ni vijana wastaarabu ,wakarimu ,washeshi ,wenye mioyo ya huruma ,upendo na uungwana mkubwa sana. Ni vijana ambao wamesaidia wengi na kufikika kwa urahisi kabisa na yeyote mwenye shida. Ni vijana ambao kwao cheo ni dhamana na utumishi kwa watu. Ni vijana ambao kwao uongozi ni kwa ajili ya kuwatumikia watu na Kugusa maisha ya watu.

Sasa katika hali ya Mpango wa Mungu wameweza kukutana Bungeni . Hii ni historia na hajawahi kutokea tangia kupata uhuru wa Taifa letu kwa watoto wa wakuu wa nchi ambao Baba zao walikuwa Ma Rais kuweza kuwepo Bungeni kwa wakati mmoja.

Ikumbukwe ya kuwa vijana hawa na viongozi wetu hawa hawapo Bungeni kwa sababu ya upendeleo au kwa kutumia majina ya Baba zao. Bali wapo Bungeni kutokana na uwezo mkubwa wa kiuongozi walionao,uchapakazi wao,kukubalika mbele ya jamii na kuungwa mkono na wengi. Ndio sababu wakaungwa mkono na wengi na kuchaguliwa kuingia Bungeni.

Kwa hakika vijana wengine tuna kila sababu ya kuiga kutoka kwa viongozi wetu hawa. Ikumbukwe Ikulu kumekuwa kama kwao nyakati za Urais wa Baba zao. Lakini pamoja na kuishi Ikulu bado ni wanyenyekevu,wenye adabu ,heshima ,utu,uungwana ,usikivu kwa watu pamoja na kuendelea kuwa pamoja na watu na kushirikiana na kila mtu bila ubaguzi. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kwa hakika hawa vijana wanastahili pongezi kubwa sana kutoka kwetu na kuendelea kuwaunga mkono.

Tuache wivu ,chuki na mioyo ya korosho. Aliyebarikiwa kabarikiwa tu . Aliyeinuliwa na Mungu kainuliwa tu. Aliyepewa kibalia na Mungu kupewa tu na wala hawezi kushushwa na mwanadamu mwenye chuki binafsi na wivu usio na Msingi.
Screenshot_20251111-193312_1.jpg

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio Picha ya Siku kutoka Bungeni ikiwaonyesha Viongozi wetu na watumishi wetu Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete pamoja na Mheshimiwa Jesca Magufuli vijana wetu wachapakazi,wacha Mungu,wapole wanyenyekevu,wasio na Makuu wala majivuno wala kiburi wala dharau kwa mtu.

Vijana ambao wamelelewa katika maadili mazuri na yenye kupendeza na kuigwa na kila mtu. Maadili ambayo huwezi hata kujua au kutambua kama ni watoto ambao Baba zao waliwahi kuongoza Taifa letu kama Ma Rais. Vijana ambao huwezi kuona au kukuta wakijikweza au kutumia Majina ya Baba zao kuringa au kujivunia au kumuonea mtu au kuvunja sheria.

Ni vijana wastaarabu ,wakarimu ,washeshi ,wenye mioyo ya huruma ,upendo na uungwana mkubwa sana. Ni vijana ambao wamesaidia wengi na kufikika kwa urahisi kabisa na yeyote mwenye shida. Ni vijana ambao kwao cheo ni dhamana na utumishi kwa watu. Ni vijana ambao kwao uongozi ni kwa ajili ya kuwatumikia watu na Kugusa maisha ya watu.

Sasa katika hali ya Mpango wa Mungu wameweza kukutana Bungeni . Hii ni historia na hajawahi kutokea tangia kupata uhuru wa Taifa letu kwa watoto wa wakuu wa nchi ambao Baba zao walikuwa Ma Rais kuweza kuwepo Bungeni kwa wakati mmoja.

Ikumbukwe ya kuwa vijana hawa na viongozi wetu hawa hawapo Bungeni kwa sababu ya upendeleo au kwa kutumia majina ya Baba zao. Bali wapo Bungeni kutokana na uwezo mkubwa wa kiuongozi walionao,uchapakazi wao,kukubalika mbele ya jamii na kuungwa mkono na wengi. Ndio sababu wakaungwa mkono na wengi na kuchaguliwa kuingia Bungeni.

Kwa hakika vijana wengine tuna kila sababu ya kuiga kutoka kwa viongozi wetu hawa. Ikumbukwe Ikulu kumekuwa kama kwao nyakati za Urais wa Baba zao. Lakini pamoja na kuishi Ikulu bado ni wanyenyekevu,wenye adabu ,heshima ,utu,uungwana ,usikivu kwa watu pamoja na kuendelea kuwa pamoja na watu na kushirikiana na kila mtu bila ubaguzi. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kwa hakika hawa vijana wanastahili pongezi kubwa sana kutoka kwetu na kuendelea kuwaunga mkono.

Tuache wivu ,chuki na mioyo ya korosho. Aliyebarikiwa kabarikiwa tu . Aliyeinuliwa na Mungu kainuliwa tu. Aliyepewa kibalia na Mungu kupewa tu na wala hawezi kushushwa na mwanadamu mwenye chuki binafsi na wivu usio na Msingi.View attachment 3500400

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Ashapiga?
 
Baba zao walikuwa marais, Mama zao wanakula pension ya Baba zao na Malupulupu kibao na sasa watoto wabunge

Alafu Wewe Mama na Baba yako wakulima maskini ambao wanalima vinyungu pale VWAWA na mtoto wao ni kondakta wa gari za vwawa kuja hapa Mbeya alafu unawasifia na kuwa chawa na shabiki wa watoto wa marais wastaafu.

Pumbavu.
 
Mimi naongea ukweli na siyo kuwasifia.
 
Back
Top Bottom