Picha: Yanga wakifanya mazoezi ulaya... Uturuki...

Picha: Yanga wakifanya mazoezi ulaya... Uturuki...

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
HIVI NDIVYO KLABU YA SOKA INAVYOTAKIWA KUWA (YANGA WAKIFANYA MAZOEZI ULAYA )






Wachezaji wa Young Africans wakifanya mazoezi leo katika Uwanja wa Fame Residence Football - Antalya Uturuki

Young Africans Sports Club imeanza mazoezi leo asubuhi katika viwanja vya Fame Footballl vilivyopo pemebni kidogo mwa hoteli ya Fame Residence Lara & Spa iliyopo kusini mwa mji wa Antalya ambapo imeweka kambi ya mafunzo ya wiki mbili.

Kocha Brandts akisaidiwa na kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razaki Siwa waliongoza mazoezi hayo yaliyoanza majira ya saa 4 kamili asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na awamu ya pili ilianza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Ratiba ya mazoezi ni mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, ambapo timu inapata huduma zote za kambi katika Hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kuanzia chakula, malazi, mazoezi ya viungo (Gym) ufukwe kwa ajili ya mazoezi ya stamina na kujenga mwili.












Kocha wa Magolikipa Razaki Siwa akiwawapa maelekezo magolikipa Said Mohamed, Yusuph Abdul na Ally Mustafa 'Barthez'

Mji wa Antalya ni maarufu katiak medani ya soka kwani kwa ripoti tuliyopewa timu zaidi ya 200 zimeshafika katika mji huu kipindi cha majira ya baridi kuja kuweka kambi zikitokea katika nchi tofauti duniani.

Wenyeji wa Young Africans Team Travel wameada sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya ambapo wachezaji na viongozi pamoja wenyeji wa mji huu watasherehekea pamoja.



Wachezaji wa Young Africans wakiwa nje ya hotel ya Fame Residence tayari kwa kuelekea kuanza mazoezi

YANGA YAWASILI Antalya IIKITOKEA Istanbul




Kikosi cha mabingwa wa kombe la Kagame mara mbili mfululizo timu ya Young Africans imewasili salama katika mji wa Antalya kusini mwa nchi ya Uturuki majira ya saaa 10:30 jioni kwa saa za afrika mashariki na kati na moja kwa moja kupolekewa na wenyeji wake kampuni ya Team Travel.

Young Africans imefikia katika hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kilomita chahce kutoka katika uwanja wa ndege wa antalya, ambapo hoteli ya Fame Residence ipo mwambaoni mwa bahari ya mediteranian.

Mwanzoni Yanga ilikuwa ifikie katika hotel ya Sueno Beach Hotel iliyopo kilometa 70 kutoka uwanja wa ndege lakini jana siku moja kabla ya safari ilifanya mabadiliko na kuamua kuhamia katika hotel ya Fame Residence.






Wachezaji wamefurahi mandhari ya hotel kwani ni miongoni mwa hotel za nyota tano katika mjii huu wa Antalya hivyo wamefariijika na kuupa hongera uongozi kwa hatua waliyofikia ya kukubaliana na mwalimu kuweka kambi ya mafunzo nchini Uturuki.





Timu itaanza mazoezi kesho asubuhi katika viwanja vilivyopo katika eneo la hotel ya fame, ambapo kwa siku timu itakua inafanya mazoezi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni.

Kuhusu hali ya hewa ni baridi kiasi na sio baridi kali kama ilivyokuwa inatangazwa na vyombo vya habari hapo awali.

Mtandao wa klabu The Official Website of Young Africans Sports Club utaendelea kuwajuza juu ya kila kitu kinachojiri nchini Uturuki.



YANGA NDANI YA ISTANBUL UTURUKI



[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]keiza na meneja wa yanga uwanja wa ndege wa
istanbul wakisubiri ndege nyingine
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
YANGA SC, mabingwa mara tano wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame wamefika salama Istanbul, Uturuki na wameunganisha ndege ya kwenda Antalya, ambako wataweka kambi.

Yanga itaweka kambi katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa Uturuki na itafikia katika hoteli ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.


Yanga iliondoka Dar es Salaam Alfajiri ya leo, saa 10:30 ikiwa na kikosi kamili; makipa; Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yussuf Abdul, mabeki Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro', Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani.


Viungo ni Athumani Iddi ‘Chuji', Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari, Omega Seme, Simon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende wakati washambuliaji ni Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerry Tegete, George Banda na Hamisi Kiiza.


Upande wa benchi la ufundi ni Kocha Mkuu Mholanzi, Ernie Brandts, Kocha Msaidizi Freddy Felix Minziro na Kocha wa makipa, Razak Ssiwa, na Maofisa wengine ni Daktari wa timu, Sufiani Juma, Meneja Hafidh Saleh, Ofisa Habari, Baraka Kizuguto Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mohammed Nyenge.




 
hongera wanajangwani kweli mmeamua kufanya kweli.
Nawapa big up uongozi pamoja na benchi la ufundi
 
Al Shaabab haamini kama yaliyosemwa yametimia, yeye anaendelea na porojo za kwenda Oman kila kukicha. Vitendo kwanza, porojo baadaye. Yanga oyee na Simba zii!
 
Nasikia mtani kaweka kambi maeneo ya vigwaza.
 
Kazi ipo kwani uwanja kama hauna vyoo nini kitafuata wakibanwa na haja ndogo?tusilaumu culture yetu ndio 'waafrika tulivyo'kwa wenzetu wa ulaya kujisaidia haja ndogo barabarani wanajifunza ukubwani kwani hata vichaka hakuna kwa wingi kama huku kwetu!!
 
halafu mchukue na ubingwa wa afrika ninyi yanga na simba mpira hatujui tunauza sura tu mimi wacha manchester united iniue
 
najivunia kuwa mwana Yanga. timu ambayo hata mwanachama mdogo kama mm akitoa ushauri wake husikilizwa na kupewa ushirikiano.

kimsingi klabu ya yanga inaweza yote haya kwani uongozi wake upo makini katika kuskiliza hoja na kuzifanyia kazi. huwa sioni tabu kupita jangwani na kudondosha neno langu kwa viongozi wa klabu. hapa hata @kikungu atathibitisha haya. halaf nipe matokeo ya maveterani nani alishinda??
 
Nnachowaomba 2 watani zangu.. Hakuna kufanya uchaguzi mwingine mwaka huu. Tukutane taifa safari hii atakuwepo yule yule pale pale ktk eneo lile lile aliyesababisha kanjibai aka Kagoda kupewa jukumu na chama kuongoza magamba fc! Chondechonde msijekumdai kanjibai timu yenu tu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mzee wa bastola anasubiri mwaliko wa kampuni ya mafuta apeleke timu Oman......!!!!!!
 
Tuache ushabiki, mtu akifanya kitu kizuri apewe sifa zake anazostahili. Kwa hili la kuwa serious na maandalizi, big up sana Yanga. Kuwa timu ni zaidi ya kupigiana pasi, ni kujenga umoja wa kiakili, kisaikolojia na kifamilia kama Yanga wanavyoelekea kufanya. Big up
 
Madeni wamelipa?? Papic Njoroge St Tom. Madeni fc

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nacikia watacheza na Galatasaray na Besiktas..
 
Tuache ushabiki, mtu akifanya kitu kizuri apewe sifa zake anazostahili. Kwa hili la kuwa serious na maandalizi, big up sana Yanga. Kuwa timu ni zaidi ya kupigiana pasi, ni kujenga umoja wa kiakili, kisaikolojia na kifamilia kama Yanga wanavyoelekea kufanya. Big up
wamechelewa, serious kujiandaa na ligi ya vodacom...wauza sura tu hawana lolote
 
Back
Top Bottom