Picha za Gaza ilivyo sasa na Gaza ilivyokuwa awali

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,678
Reaction score
27,653
Screenshot_20250320-184137_1.jpg

Trump alisema Gaza imekuwa kuzimu, hakufai kwa maisha ya mwanadamu.

Hamas wanasifiwa na wajahidina wasiofikiria kwamba wameshinda vita. Je huu ndio ushindi sasa walioupata mbele ya Israeli?. Hamas wamefanya 60% ya mji wa Gaza kuwa magofu na maganjo. Na 40% imekuwa kama mashamba. Gaza ina vilema wa vita zaidi ya laki moja na imepoteza watu zaidi ya elfu 50. Zingatia Gaza ina wakazi milioni mbili, na 1.5M walikuwa wakimbizi. Walishauriwa wakae chini na Israeli na wakapewa muda zaidi ya mwezi ili kuachia mateka, wakagoma na kuchagua vita.

Laiti wangesoma au kufuata shauri hili, leo Gaza ingekuwa hai. 👇

[28] Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? [29] Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, [30] wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza. [31] Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini? [32] Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali. Lk 14:28-32 SUV

Wao wameamua kuchagua jihadi. Haya Israeli imerudi Gaza tena kwa kishindo. Na kibaya zaidi raia walikataa shauri la Waarabu wenzao na wakaanza kurudi Gaza iliyobomoka. Sasa wameanza kukimbia tena Gaza sababu ya mashambulizi ya Israeli. Inauma sana. Ila laiti Wapalestina wangekuwa na muda wa kufikiria, wangeikataa Hamas maana muhujumu wa Gaza ni Hamas na sio Israeli. Angalia makazi ya Wapalestina wengine ambao wapo chini ya Mahamud Abbas, maisha kwao yanaendelea tu kwa amani na wengine ni waajiriwa katika serikali ya Israeli.

Trump aliomba aijenge Gaza kwa miaka 5 ila ombi lake lilikataliwa na Hamas.

Na Jeff
 
Haya ndio aina ya maisha ya wana Gaza

Kuna Muislamu mmoja nilimsikiliza nikaona hoja yake ina mashiko. Alisema kwajili ya usalama wa raia wa Gaza, waondoke Gaza kunusuru maisha yao, wabakie wapiganaji tu hapo. Trump naye alipoingia madarakani naye akatoa hoja hiyo hiyo. Pia jana nimemsikiliza rais wa Somali land naye katoa hoja kama hiyo na kuwakaribisha watu wa Gaza waje Somali land kwa usalama wao.

Pasipo hivyo wataangamia, na Hamas hawawezi kuwasaidia zaidi ya kuipeleka Gaza kuzimu. Ulimwengu haupo na Gaza, wamekalia maneno tu na huruma ya machozi ya Mamba kwa Gaza. UN (dunia) imeshindwa kabisa kabisa kuzuia au kuleta amani ndani ya Gaza, maana kidole cha mwisho cha Israeli kimekuwa kinene kuliko kiuno chao.

Kuwataka wa Gaza waendelee kukaa hapo, ni kupitisha mauti yao. Wakazi wa Ukraine hasa wamama na watoto walipewa hifadhi nchi nyingine.
 
Mwanzo kipindi kimbari kimeshika hatam watu 40000 niliwalaan Israel ila kwa sasa hata huruma kwa gaza Sina naona kama ni wajinga tu acha wafe kwa ujinga wao
Hongera nyie wagalatia mtakao ishi milele.
 
View attachment 3277683

Trump alisema Gaza imekuwa kuzimu, hakufai kwa maisha ya mwanadamu.

Hamas wanasifiwa na wajahidina wasiofikiria kwamba wameshinda vita. Je huu ndio ushindi sasa walioupata mbele ya Israeli?. Hamas wamefanya 60% ya mji wa Gaza kuwa magofu na maganjo. Na 40% imekuwa kama mashamba. Gaza ina vilema wa vita zaidi ya laki moja na imepoteza watu zaidi ya elfu 50. Zingatia Gaza ina wakazi milioni mbili, na 1.5M walikuwa wakimbizi. Walishauriwa wakae chini na Israeli na wakapewa muda zaidi ya mwezi ili kuachia mateka, wakagoma na kuchagua vita.

Laiti wangesoma au kufuata shauri hili, leo Gaza ingekuwa hai. 👇

[28] Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? [29] Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, [30] wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza. [31] Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini? [32] Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali. Lk 14:28-32 SUV

Wao wameamua kuchagua jihadi. Haya Israeli imerudi Gaza tena kwa kishindo. Na kibaya zaidi raia walikataa shauri la Waarabu wenzao na wakaanza kurudi Gaza iliyobomoka. Sasa wameanza kukimbia tena Gaza sababu ya mashambulizi ya Israeli. Inauma sana. Ila laiti Wapalestina wangekuwa na muda wa kufikiria, wangeikataa Hamas maana muhujumu wa Gaza ni Hamas na sio Israeli. Angalia makazi ya Wapalestina wengine ambao wapo chini ya Mahamud Abbas, maisha kwao yanaendelea tu kwa amani na wengine ni waajiriwa katika serikali ya Israeli.

Trump aliomba aijenge Gaza kwa miaka 5 ila ombi lake lilikataliwa na Hamas.

Na Jeff
Gaza kumefanywa uhalifu mkubwa wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
 
Kwanza walianza October 7

Pili wameambiwa wa release mateka vita viishe hawataki sasa hao unawasaidiaje
Hawasaidiki hao watu! Ungeenda Russia, China, or NK uteke watu zaidi ya elfu huo mtiti ungekuwa historia!
 
Mtoa mada fuatikia mambo Wayahudi sio waadikifu hata kidogo , unasema kule West Bank Kuna Amani wakati wanaoishi kama jela kila siku wanafanyiwa Fujo , nyumba zao zinabomolewa huku Zionists settlers wakiongezeka.

West Bank huko Kuna Hamas ?
Screenshot_2025_0320_214831.jpg
 
Kwanza walianza October 7

Pili wameambiwa wa release mateka vita viishe hawataki sasa hao unawasaidiaje
Umefanya mgogoro kama umeanzia October 7 wakati ndio maisha Yao ya kuonewa kila siku wawe wametulia au vipi ni lazima chokochoko zianze kutoka upande hasimu.

Unafuatilia chanzo Cha Cease Fire deal kugoma ? Wayahudi walikuwa hawatimizi makubaliano ya kuruhusu misaada ya kibinadamu kupita ambayo ipo kwenye makubaliano ya kuachiwa mateka.
 
Chuki ya kidini imewapofusha macho. Wenyewe wanaona jihad ni haki yao na kufa kwa ajili ya allah ili waende peponi ni wajibu wao.
 
Wameamua kuchagua njia ya vita kutatua matatizo yao waendelee kupambana
 
Back
Top Bottom