hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 18,678
- 27,653
Trump alisema Gaza imekuwa kuzimu, hakufai kwa maisha ya mwanadamu.
Hamas wanasifiwa na wajahidina wasiofikiria kwamba wameshinda vita. Je huu ndio ushindi sasa walioupata mbele ya Israeli?. Hamas wamefanya 60% ya mji wa Gaza kuwa magofu na maganjo. Na 40% imekuwa kama mashamba. Gaza ina vilema wa vita zaidi ya laki moja na imepoteza watu zaidi ya elfu 50. Zingatia Gaza ina wakazi milioni mbili, na 1.5M walikuwa wakimbizi. Walishauriwa wakae chini na Israeli na wakapewa muda zaidi ya mwezi ili kuachia mateka, wakagoma na kuchagua vita.
Laiti wangesoma au kufuata shauri hili, leo Gaza ingekuwa hai. 👇
[28] Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? [29] Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, [30] wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza. [31] Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini? [32] Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali. Lk 14:28-32 SUV
Wao wameamua kuchagua jihadi. Haya Israeli imerudi Gaza tena kwa kishindo. Na kibaya zaidi raia walikataa shauri la Waarabu wenzao na wakaanza kurudi Gaza iliyobomoka. Sasa wameanza kukimbia tena Gaza sababu ya mashambulizi ya Israeli. Inauma sana. Ila laiti Wapalestina wangekuwa na muda wa kufikiria, wangeikataa Hamas maana muhujumu wa Gaza ni Hamas na sio Israeli. Angalia makazi ya Wapalestina wengine ambao wapo chini ya Mahamud Abbas, maisha kwao yanaendelea tu kwa amani na wengine ni waajiriwa katika serikali ya Israeli.
Trump aliomba aijenge Gaza kwa miaka 5 ila ombi lake lilikataliwa na Hamas.
Na Jeff