Picha za WAJUMBE : Je, unayo moja? Hebu weka hapa tuwaone...

Picha za WAJUMBE : Je, unayo moja? Hebu weka hapa tuwaone...

Mjumbe akiuliza "NGAPI UKOO""
255679363822_status_ee45e78138324b7699f0d4d5cda58010.jpg
 
SHAIRI LA WAJUMBE[emoji2][emoji2][emoji2]

Simu walinipigia,
Sifa zangu kunipatia,
Wakanisihi nitie nia,
Wajumbe sio watu wazuri

Walisema nakubalika,
Nitapita bila shaka,
Kura zao walinipa uhakika,
Wajumbe sio watu wazuri

Mara nyingi tulikutana,
Mipango tuliweka bayana,
Nilipambana usiku na mchana,
Wajumbe sio watu wazuri,

Ukumbini tulipoingia,
Sera kuwamwagia,
Kwa kweli walishangilia,
Wajumbe sio watu wazuri,

Kura zikawekwa mezani,
Kila mtu na yake mkononi,
Walichonifanya wajumbe sikuamini,
Wajumbe sio watu wazuri

Sikupata hata kura moja,
Hata ya wale tuliokuwa pamoja,
Ningejinyonga ningekuwa kihoja,
Wajumbe sio watu wazuri
 
SHAIRI LA WAJUMBE[emoji2][emoji2][emoji2]

Simu walinipigia,
Sifa zangu kunipatia,
Wakanisihi nitie nia,
Wajumbe sio watu wazuri

Walisema nakubalika,
Nitapita bila shaka,
Kura zao walinipa uhakika,
Wajumbe sio watu wazuri

Mara nyingi tulikutana,
Mipango tuliweka bayana,
Nilipambana usiku na mchana,
Wajumbe sio watu wazuri,

Ukumbini tulipoingia,
Sera kuwamwagia,
Kwa kweli walishangilia,
Wajumbe sio watu wazuri,

Kura zikawekwa mezani,
Kila mtu na yake mkononi,
Walichonifanya wajumbe sikuamini,
Wajumbe sio watu wazuri

Sikupata hata kura moja,
Hata ya wale tuliokuwa pamoja,
Ningejinyonga ningekuwa kihoja,
Wajumbe sio watu wazuri
[emoji16][emoji16][emoji16] wajumbeeeee
 
 
 
Huu mtindo wa uteuzi wa hiki chama unatoa burudani sana wakati watu tunajiandaa kwa uchaguzi mkuu ambao haki ni nadra sana kutendeka.

Ni sawa na beberu kulishwa majani mazuri na yenye kunukia kabla ya kuchinjwa.
 
 
Back
Top Bottom