SHAIRI LA WAJUMBE[emoji2][emoji2][emoji2]
Simu walinipigia,
Sifa zangu kunipatia,
Wakanisihi nitie nia,
Wajumbe sio watu wazuri
Walisema nakubalika,
Nitapita bila shaka,
Kura zao walinipa uhakika,
Wajumbe sio watu wazuri
Mara nyingi tulikutana,
Mipango tuliweka bayana,
Nilipambana usiku na mchana,
Wajumbe sio watu wazuri,
Ukumbini tulipoingia,
Sera kuwamwagia,
Kwa kweli walishangilia,
Wajumbe sio watu wazuri,
Kura zikawekwa mezani,
Kila mtu na yake mkononi,
Walichonifanya wajumbe sikuamini,
Wajumbe sio watu wazuri
Sikupata hata kura moja,
Hata ya wale tuliokuwa pamoja,
Ningejinyonga ningekuwa kihoja,
Wajumbe sio watu wazuri