KWELI Picha zinazoonyesha wanajeshi wa Marekani wamekamatwa nchini Iran zimetengenezwa kwa kutumia Akili Unde

KWELI Picha zinazoonyesha wanajeshi wa Marekani wamekamatwa nchini Iran zimetengenezwa kwa kutumia Akili Unde

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
1772965445829.png
645648221_2116113295890484_6027495960736580241_n.jpg
 
Tunachokijua

Kumekuwepo na machapisho yanayosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram, Facebook na X (zamani Twitter) yakidai kuwa wanajeshi wa vikosi maalum vya Marekani, maarufu kama Delta Force, wamekamatwa na vikosi vya jeshi la Iran. Machapisho hayo pia yanadai kuwa wanajeshi hao walikuwa sehemu ya kikosi kilichotumwa na Rais wa Marekani Donald Trump mnamo Januari kwa ajili ya operesheni ya kumkamata kiongozi wa Venezuela, Nicolás Maduro, mjini Caracas.


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji kuhusu kuhusu picha zinazosambaa zikidai kuonesha wanajeshi wa Marekani wakikamatwa nchini Iran umebaini kuwa picha hizo zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde

Aidha Rais Trump, alipofanya mahojiano na vyombo vya habari, alitupilia mbali wazo la kutumia wanajeshi wa ardhini katika vita vinavyoendelea akisema jambo hilo linahita kufanyika kwa kuzingatia sababu muhimu ya kufanya hivyo.

Marekani na Israel zimetajwa kujadili uwezekano wa kutuma vikosi maalumu kwenye vituo vya nyuklia vya Iran ili kuhakikisha usalama wa uranium ulioboreshwa. Endelea kufuatilia maendeleo ya hivi karibuni katika mzozo wa Iran na mkakati wa kijeshi wa Marekani.

Kwa mantiki hiyo, picha zinazoonyesha wanajeshi wa Marekani wakikamatwa na jeshi la Iran hazina zinapotosha uhalisia kwa kuwa hakuna ushahidi wa kuwepo kwa operesheni ya ardhini ya jeshi la Marekani nchini Iran hadi sasa.

Pia hakuna chombo chochote kutoka Iran kilichothibitisha kuwakamata wanajeshi wa marekani katika vita inayoendelea.

Sanjari na hayo kupitia nyenzo za kidigitali imebainika picha hizo zimetengenezwa kwa kutumia Google AI. Picha hizo zimeonekana kuwa na alama maalum (watermark) pamoja na viashiria vya kidijitali vinavyotumika kutambua maudhui yaliyotengenezwa kwa AI.​

View attachment 3554792
View attachment 3554796


1772964286492-png.3554799

Attachments

  • 1772964129784.png
    1772964129784.png
    1.4 MB · Views: 36
Back
Top Bottom