KWELI Pierre Liquid ni mgonjwa, asema yupo nyumbani anajiuguza (Agosti 11, 2022)

KWELI Pierre Liquid ni mgonjwa, asema yupo nyumbani anajiuguza (Agosti 11, 2022)

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Mchekeshaji maarufu aliyejipatia umaarufu wake kupitia mitandao ya kijamii, Pierre Liquid amelazwa Hospitali ya Muhimbili Mwaisela wodi namba 6 iko ghorofa ya pili.

Aidha inaelezwa kuwa haijafahamika mpaka sasa Piere anasumbuliwa na ugonjwa gani.

1660289545233.png
 
Tunachokijua
Konki Liquid. Pierre. Mama nakufa. Chii. Ni utambulisho wa mwanaume huyu aliyejizolea umaarufu siku za hivi karibuni.

Huyu ni Peter Mollel, umaarufu wake uliibuka baada ya video iliyomuonyesha akisema “mama nakufa” kuzagaa mitandaoni mwishoni mwa mwaka 2018.

Amepitia mambo mengi ikiwemo kupata ajali ya kuvunjika mguu, na sasa inasemekana yuko hoi taabani akiugua.

Ukweli upoje?
Taarifa rasmi kutoka kwa Pierre Liquid ambaye yeye mwenyewe ameamua kuzungumza Agosti 30, 2022, amesema:

"Ni kweli ninaumwa, afya yangu haipo sawa na kwa sasa nipo nyumbani. Taarifa zaidi siwezi kueleza lakini afya yangu siyo nzuri."

Piere Liquid ni mfanyabiashara wa samani, hana watoto na hajaoa.
Mwamba mtu poa sana naumbuka 2019 alitupigia promo kwenye kakibanda chetu cha vifaa vya simu, ilitupush sana enzi hizo
 
Ushaona wapi mtu anayekunywa namna ile ili atoke akabaki salama? Labda atoke kabisa dunia kwa kuharibu miundombinu ya mwili wake. Kuna mambo hayana longolongo, kama afya.
Kuna wazee ni walevi umbwa Toka wakiwa watoto tena sio bia ni gongo na pombe chafu nyingine lakini Sasa wanamika 70 na bado walevi njoo vingunguti utajionea kifo na maradhi ni fumbo kwanza sioni kama huyo jamaa kama alikuwa mlevi kupitiliza
 
ndugu….wewe mtakie Heri tuu katika changamoto zake za afya. Hayo ya figo hata wasiokunywa Pombe na wanashinda gym….zinaharibika tuu. wangapi wameishi miaka 90 na wanavuta sigara tangu utotoni? Wangapi wametangulia mbele ya haki hata Nyama hawagusi……red meat tunaambiwa. Reality is….kila mtu ana namna yake ya kupigania afya. Mwisho wa siku….uhai anatoa Allah.
umeongea kweli kabisa
 
Back
Top Bottom