Elections 2010 Piga kampeni kwa simu

Elections 2010 Piga kampeni kwa simu

[/color]


nimeipenda sana hii imatia moyo , nitaendelea kuwashawishi wengi zaidi ili wote tumpe kura dr slaa

fanya hivyo na mwambie na mwenzako afanye hivyo, si wakati wa kulala
 
Hebu mwerevu mmoja atuwekee hapa mfano wa text SMS characters zisizidi 140 ili tugelezee na kuanza kuzituma mapema kesho.
 
ni vigumu kuamini kwamba ndugu zako wote 14 wamekuambia ukweli wakati kura ni kitendo cha siri. Mtu anaweza kufika pale na akampa kura yake Kikwete au mgombea mwingine yeyote. Ningekuwa mimi kwa kutumia hesabu za yamkini (probability) hapo ungesema una kura 8 na zingine sita huna uhakika nazo kwa sababu ya tabia ya binadamu usiri na kubadilikabalika( kigeugeu).

kazimoto, maisha ya watu yamekuwa magumu, wa2 wengi wamechoka na ufisadi, kuhusu hapa ofisini, hawa watu niliokueleza wote, ni wapenda mabadiliko, na sio vigeugeu, na wao wanonyesha mapenzi mema kwa slaa, kuliko hata mimi, na mara nyingi wameni2mia sms, na wengi zaidi walikasirishwa na jk, kudharau wafanyakazi.

Kwa mfano baba yeye ndo mara kwa mara huwa anani2mia ujumbe kuhusu chadema, na kunihamashisha , nisimpigie jk,
 
nitawashawishi wanakwaya kumpigia kura slaa baada ya mazoezi,kwenye daladala nitaanza kujaribu kuanzisha mjadala
 
Hizi simu naamini zinaweza kufanya kazi kubwa kuliko yale mabango ya barabarani. Huwezi amini habari hii, ila ni kweli tupu nayo imenistajabisha sana. Mama yangu mimi ana umri wa miaka 75 na yupo kijijini juzi kushinda jana kaniforwadia sms ya ile sala ya Jk ya jina lako ni usanii mtupu. Ndipo kwa mshangao nikamtwangia nikamwuliza ameipataje kasema nimetumiwa na mtu nisiemjua. Basi nikataka kudodosa amesimama upande gani kabla sijaenda mbali yeye ndio kaniwahi kwamba kura yake mwaka huu anampa Silaa angependa na mimi nifanye hivyo. Nimemweleza kuwa mimi na mke wangu tutampa Dr slaa, ndipo akaendelea kuwa mtumie na mdogo wako ampigie Silaa nikamwambia nilisha mtumia na alinijibu kuwa kura yake ni kwa Slaa hata kama nisingemweleza. Habari hizi zimenipa moyo sana kuona bibi vizee wa kijijini ni wanamageuzi. Pia naungana na mchangiaji mmoja aliyetaka sms i-draftiwe isiyozidi tarakimu 140 ya kushawishi kuhusu kumpigia Dr Slaa kura ili tuitume sote kwa ndg jamaa na marafiki zetu tunaowafahamu. HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE. Dr SLAA NI RAIS WA AWAMU YA TANO TZ!!
 
Mwambie Mama yako, Baba yako, Shangazi yako, Mjomba wako na Hata Jirani Zako kwamba kama wao Walisoma Bure kwa Korosho na Kahawa, je itakuwa sasa hivi tunachimba Madini, tunachimba gesi na sasa tunachimba Uranium? Elimu Bure inawezekana, Wasipoteze hii fursa

CHAGUA MABADILIKO, CHAGUA CHADEMA
 
Kwa wale wanaotumia Zain kuna huduma ya bure ya sms 100 kila siku usiku baada ya saa 6 kamili. Tumia nafasi hiyo usilale. Tuma message kwa watu 100 unaowafahamu na kuwakumbusha kwamba nchi inaelekea katika mabadiliko makubwa na haya mabadiliko yatakuja kwa kumuingiza ikulu ya Tanzania Dr Slaa. CHAGUA DR SLAA CHAGUA CHADEMA CHAGUA MABADILIKO CHAGUA MAENDELEO YA TANZANIA.

TIGO wana huduma kama hii... Unatuma Neno Extreme SMS kwenda 15313... unapata Message 100 kila siku... Ila wanakata sh. 500 kiasi ambacho sidhani kama ni kikubwa kulingana na ukombozi wa nchi yako...

Mi nawashawishi waumini wangu kila siku... wameahidi mabadiliko...

Pipoz....
 
mimi si mzuri sana katika kudraft msg zenye ushawishi, kama kuna mtu anaweza kuweka template hapa, nami nitazituma leo kwa watu 100 kupitia laini yangu ya tigo
 
Baada ya kusoma hii sredi, nimetuma msg kwa watu wote kijijini kwangu wenye simu za mkononi, nimepata majibu ya Ndio kwa Slaa na badi msg zinaendelea kuingia. Pamoja tunaweza
 
mimi si mzuri sana katika kudraft msg zenye ushawishi, kama kuna mtu anaweza kuweka template hapa, nami nitazituma leo kwa watu 100 kupitia laini yangu ya tigo

Wakinge uwapendao na CCM, vunja ukimya zungumza na mwenzako. Chagua CHADEMA, okoa Taifa lako na mafisadi pamoja na ahadi hewa! Badili mfumo wa kura yako. Tanzania bila CCM INAWEZEKANA. Imedhaminiwa na wanaopenda maendeleo, Kwa msaada wa vijana wa Kisasa!

JAMANI, NIMEJARIBU KUI-DRAFT HII, RUKSA KUI-EDIT KAMA MTAONA INAFAA, BASI NADHANI TUNAWEZA KUITUMIA, MIMI NIMESHAITUMA KWA WATU WANGU WA KARIBU ZAIDI YA ISHIRINI!!
 
.Mh Kakobe namsifu sana kwa kutoa elimu ya uraia nzuri sana....kwa ambao hawakuona waangalie star tv kesho saa tatu kamili usiku na unaweza kutumia hiyo kuwaconvince watu wengine..wambie waangalie tv muda huo basi na baada ya lipindi watakuwa wamebadilika.....
Mh Kakobe haongei kama mtu wa kawaida bali ni Upako usio wa kawaida na impact yake ni kubwa sana....
KURA LAZIMA ZITATOSHA TU....just play your part ikiwa ni pamoja na kuchangia chama kipate fedha kiendelee na kampeni...
Nilitaza kipindi, aisee kaelimisha sana naametoa dvd zinauzwa nilicopy DVD 20 nikawa wawia ndungu na jamaa ambao walikuwa wagumu lakini baada ya kuitazama naona wamelainika ila mnisamie kwa kukopy dvd kakobe...
 
Ndugu wana Jamvi, hatupaswi kulala bila ya kupigia Simu babu zetu, mama zetu na ndugu jamaa na Marafiki na kuwakumbusha juu ya Mabadiliko tunayoyataka kuyafanya kesho

Kabla ya kulala hakikisha umepiga simu au kutuma sms ya Ujumbe wa mabadiliko kwa ndugu jamaa na marafiki, Kwa sisi Mwisho wa kupiga kampeni ni Kesho saa 1800 jioni. Kampeni ziendelee mpaka kwenye mistari ya Foleni

Asanteni sana nawatakia Uchaguzi mwema


Pipooooooooooooooooooooooooz.......


"Mabadiliko ya kweli ni yale tunayojiletea na Si yale tunayoyangojea" M.M. Mwanakijiji
 
Asante sana Lisa naona umeelewa Somo

<LI class="uiUfiComment comment_1697954 ufiItem ufiItem"> Lisa M Rockefeller All Tanzanian's both in and outside the country, please take a phone call one or two of your family members, let them know their vote counts, and they should send the message to all they know that Kikwete does not deserve a second chance, dont be intimidated, your ballot power is more powerful than their tear gases. i have just recived a text from a friend in Mumbeya that, they have been tear gased. this it the family that kept me in Tanzania, and their son locked up 7 minutes ago · LikeUnlike
 
Back
Top Bottom