Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mabingwa watetezi Young Africans (Yanga SC) watashuka dimbani Machi 5, 2026 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Black Stars bila wachezaji Watatu muhimu, jambo linalopelekea pigo kubwa kwa matumaini yao ya kutetea ubingwa.
Yanga watakuwa bila kiungo wao, Pacome Zouzoua, beki Dickson Job, na kiungo Mohammed Damaro. Wakati Pacome na Job wako nje kwa sababu ya majeraha, Damaro anatumikia adhabu ya mechi moja baada ya kuonyeshwa kadi tatu za njano. Vilevile Yanga wataendelea mkosa mshambuliaji wao Clement Mzize aliyetonesha jeraha lake wakati yupo hatua za kurejea Uwanjani na kupelekwa Afraika Kusini kwa matibabu.
Pacome amekuwa nje tangu alipopata jeraha la bega wakati wa mechi ya Kombe la Mabingwa Afrika dhidi ya JS Kabylie Februari 15, 2026 ikiwa mechi yake ya tano mfululizo kukosekana.
Licha ya wachezaji hawa kutokuwepo, Yanga bado wako kileleni mwa Lligi wakiwa na Alama 29 baada ya mechi 11. Singida Black Stars wako nafasi ya 9 wakiwa na Alama 19.