Pikipiki aina ya TVS inakunywa mafuta balaa

Pikipiki aina ya TVS inakunywa mafuta balaa

JMWAKA

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2012
Posts
739
Reaction score
652
Salaam waungwana mafundi Wa ukweli Na wale makanjanja mnaotengeneza hiki huku mnaaribu kile ili turudi kwenu Mara kwa Mara salaam sana

Jama Nina pikipiki yangu aina ya TVS cc150 cha kushangaza kama mwezi sasa hivi inakula mafuta sana mwanzoni nikiweka Lita 2 natumia Siku nzima Na kesho asubuhi inanibeba hadi mzigoni lakinj sasa zaidi ya Lita 3 Na asubuhi lazima niweke mafuta nikitoka nyumbani

Naomba msaada Kwa ushauri tafadhali
 
Au walichezea Carburetor?
 
Sorry na mimi napindisha kidogo mada..... Samahani kwa Dar ni duka gani wanauza vifaa vya pikipiki aina ya TVS King 125HLX kwa bei nafuu?
nipe orodha yako inbox nikusaidie mkuu!..
 
Jf inaelekea kupoteza radha yake kwa ujinga wa watu wachache waliotoka huko Facebook.

Mkuu mtoa mada: fanya kununua 'piston rings'mpya ikafungwe hiyo chombo alafu ulete mrejesho hapa.
Hapana TVS ndio pikipiki bora na ngumu zaidi Tanzania.
Haitakiwi kuibadiri Piston Ring hizo Ring huwa ni stable sana hata miaka 3 bila zigusa zinakaa!..
TVS haiguswiguswi Piston ring, Mkono, Block wala chochote cha kwenye Engine mpaka ipite mwaka 1 au miaka 2.
Cha kufanya aende kwa fundi amsafishie Carbulator yake na acheki Spark Plug kama chafu asafishe au anunue TVS Genuine Plug nyingine!. Akishasafishiwa aanze ikadiria pikipiki ni kwa umbali gani inakunywa mafuta (HLX150 ni 55Kms - 60Kms, HLX125 ni 65Kms - 70Kms per 1ltr).
Kingine aangalie Oil anayotumia anatakiwa tumia 20W50 mafundi wengi wa mtaa wanatumia 20W40 ambayo ni special kwa gari (laini)!.
JMWAKA ukifanya yote hayo na tatizo bado nitafute PM!.
 
Hizi zinakuwa na miss ya ajabu mafundi wengi wamechemsha na ndio sababu ya kutumia mafuta mengi
Ishu ni Plug. usiruhusu fundi aguse block, wala Valve itakula kwako. na vifaa ukibadirishiwa vibebe ni deal sana huwa haviharibiki to the extent.
 
Back
Top Bottom