Pikipiki gani ina pulling machine ya kunifikisha CONGO DRC na kurudi Dar?

Pikipiki gani ina pulling machine ya kunifikisha CONGO DRC na kurudi Dar?

Tafuta Yenye Cc 250,,inatosha sana XLR n nzuri au kawasaki,,,maana inahimili umbali mrefu bila kuchemka,,ila jitaidi kupumziaka
 
Nina experience ya kusafirii na pikipik kwa masafa marefu,trip ya mwisho nimetoka bukoba mpaka hapa arrusha,pikipiki nayotumia na honda baja 250cc,kwa kawaida safari na pikipiki si ngumu sana kama vile watanzania wengi wajuavyo bali ni experience za kidereva na umahili wa pikipiki uunayotumia,vivyo hivyo ugumu wa safari huja pale unapotumia pikipiki ndogo kwa safari ndefu ndefu,mfano unatumia sanlg toka dar mpaka mwanza,hapo lazima uchoke na uchukue uendako.kiukweli inahitaji experience,mood.na some addittional driving technique.nakushauri kama unataka kusafiri kwenda congo plz use honda 250cc iwe xl hapo utaenjoy kabisa kwakuwa hata ulaji wake wa mafuta ni mzuri,pia ina uwezo wa kutembea km 600 pasipo kuipumzisha,
 
Wakuu,

Natarajia kwenda Congo kwa usafiri wa pikipiki na baadae kurudi tena Dar, je ni pikipiki gani ina uwezo wa kutembea spidi na kuhimili changamoto zote za njiani mpaka Congo?

Wataalam wa pikipiki nijuzeni hapa
"VESPA"
 
Tafuta pikipiki kuanzia cc 500 kwenda juu.Hakikisha unavaa nguo nzito za kukabiliaba na baridi.Jitahidi kutembea mchana tu na ucku upumzike.Unaweza kabisa kwenda na kurudi.Mm nilishawahi kutumia DT 125 Suzuki toka Dar to Singida nilifika saa 6 ucku toka asubuh kwa sababu kuna muda inabidi uipumzishe kwa angalau nusu saa.
Dar singida cku nzima..,hukuwa unaijua DT125.,hii pikpik ni 2T..,huhitaji kupumzika.,cku nyingine funga kimzigo nyuma kama kg 50.,utaipenda na utakuwa kama unateleza barabarani..,Mm Kilombero,Chalinze,Segera,Lushoto nimetumia masaa 4.45
 
Hapa kuna harufu ya msiba! hawa vijana wa kileo walivyo walaini watawezea wapi! kesho ndugu zako watakuja hapa kulizia ulipo ubalozi wa Tanzania nchini Congo kuna mwili wa kijana wao amedanja unatakiwa kurudishwa Tz! Tafuta usafiri mbadala

Ha ha ha, hivi kuna watu wanajua K 4 LIFE mzee wa Mikumi yuko seriuos eeh, tena mnampa jamaa ushauri kabisa.
 
mtu asikutishe mie ni mmoja ya watu wanaotumia pikipiki kusafiri masafa makubwa....safari ya mwisho na fupi nimetoka moshi to dar...nimefika saa saba kwa kutumia cc250 na mwezi huu nategemea kwenda nayo ngara kagera! cha muhimu ni kujiamini na nidhamu ya barabarani!
 
Back
Top Bottom