Pikipiki gani inanifaa kwa matanuzi ya hapa na pale katika maisha?

Pikipiki gani inanifaa kwa matanuzi ya hapa na pale katika maisha?

Joined
Jul 8, 2017
Posts
86
Reaction score
73
Habari wadau, sina uhakika kama jukwaa hili linafaa kwa hoja yangu hivyo natanguliza samahani kwa atakayekwazika.

Nimefikiria na kuamua niishi mbali na kituo cha kazi na niwe nakuja na usafiri wangu binafsi kuliko kukaa karibu na kituo cha kazi. Baada ya kufikiri sana, nimekuja na wazo la kutafuta usafiri wa pikipiki yenye uwezo wa kusafiri masafa marefu kwa speed nzuri lakini pia isiyokula mafuta sana, na inayoweza kubeba mizigo hasa kutoka mashambani (nikiwa weekends nafanya shughuli binafsi).

Ni pikipiki mnanishauri ninunue na kwanini?
 
Kama ni sehemu yenye mchanga na utelezi hasa kipind hch cha mvua .
Boxer itakuwa nzuri zaidi. Inauwezo wa kihmili mchanga na utelez zaid ya hz nyingne hasa tvs.

Boxer domo la mamba ni nzur zaid n imara zaid kuliko boxer HD.

ALL the best
 
Pikipiki zimekaa kiboda boda hapana aiseh labda mtoa mada atapenda japo mimi pia nahitaji
Mkuu we unapenda zipi maana hizi za cc 150 below nyingi ni zimekaa kibodaboda. Labda high class kuanzia cc 250 huko ndizo za kifalme. Mimi sitaki hizo maana sitaki kuwa mtumwa wa vituo vya mafuta. Nataka nikiweka full tank nikae angalau wiki au zaidi. Kama una idea na pikipiki za Aina hii karibu sana.
 
Back
Top Bottom