Pikipiki ya 110cc naweza kusafiri nayo umbali mrefu?

Pikipiki ya 110cc naweza kusafiri nayo umbali mrefu?

Dar- Moro nimeenda mara kibao changamoto ipo maeneo ya uzomozi zone kuna baridi na upepo.
Mwaka jana nimesafiri na pikipiki ya Sanlg choka mbaya toka maeneo ya Usevya nikapita kwenye mbuga ya katavi nikahunga strike,mpanda ,uvinza,kasulu huko kote skikutana na check point wala polisi nilipo fika kibondo sasa kuna kibelia fulani nikikutana na afande mjaluo analazimisha rushwa yaani njaa mbaya baada ya hapo nikaanza kuhitafta buhigwe na Kakonko nafika Kakonko spoketi yote stadi na meno vimeisha fundi akafunga Fasta nihitafte Nyakanazi jioni giza linaingia nikalazamisha kufika Biharamulo ni saa tatu usiku nimejaa vumbi kugoma kuna vumbi balaa nikalala asubuhi saa moja nikaanza safari ya Muleba barabarani nilikua nakutana na manyani yanadharau haya pishi huko kote hakuna usumbufu kama kule kibondo belia ya Biharamulo askari yupo poa sana baadae kasindaga Muleba nikashuka zangu Nshamba nikasalmia then nikahitafta kamachumu ,rubale kufika kasikisi nikagongana na bodaboda bhana safari yangu ya katolo ikawa imefikia hapo nikarudi izibya hospitalini kutibiwa mguu kwanza mafuta na gharama yote haikufikia laki na nusu.
Hii safari ngumu na hinakuhitaji kubwa moyo Mugumu na kutanguliza Mungu
Ukanda huu wa mikoa ya magharibi una mapoli mengi na usiku kuna mambo mengi sio yote naweza sema humu
Baadae pikipiki niliacha nikarudi na basi la ruchoro ya mwanza Sumbawanga
Aisee pole Sana...

Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app
 
Wataalam, kwema?

mimi sio Mzuri sana wa chombo cha moto kwenye ufundi zaidi ya kuendesha tu.

Nina Pikipik yangu Aina ya Lifo (wengi wanafananisha na kibao cha mbuzi) ina 110cc iko Vizuri sana (kwa ajili ya matumizi yangu tu)

Lakini siku zinavyozidi inanihamasisha kusafiri nayo mikoani. Wiki iliyopita nilisafiri nayo kutoka Dar hadi Chalinze nilitumia masaa matatu kwa Speed ya 50 hadi 60 (nilisimama mlandizi kupata supu kidogo) nilikuwa nafika speed 80 pale napo overtake tu.

Kuna mtu aliniambia chombo chochote kinachotumia injini kama unaenda mbali hakikisha usiilazimishe mwendo.

Siku hiyo hiyo nikatoka Chalinze to Dar niliondoka chalinze saa 10 kamili jioni nonstop nikafika Dar saa 12 hivi maana nilikutana na Jam jam.

Kesho yake nikabadilisha oil so pikipiki nzima kabisa na sijaona tatizo lolote.

Sasa baada ya safari ya Dar to Chalinze na Chalinze to Dar nimeanza kunogewa kusafiri na pikipiki kwenda nayo mbali, nawaza kwenda nayo dodoma au Tanga kutembea tu na usafiri wangu.

Je, wataalam naweza kusafiri umbali mrefu kama Moshi au dodoma na Pikipiki 110cc.

(picha ndo mwonekano wa Pikipik yangu ilivyo)View attachment 2352833
Unatafuta kifo wewe, hiyo si ya safari ndefu na pia huna uzoefu.
 
Nafanya kazi kariakoo naishi chalinze natumia boxer 150 mdomo wa mamba kila siku naenda job na kurudi, so mimi naona ukiipata ya design hii utafika vizuri tu
 
Unatafuta kifo wewe, hiyo si ya safari ndefu na pia huna uzoefu.

mtaalam uzoefu hauji kwa kusema sina uzoefu ata hao wazoefu walianza safari zao wakiwa 0KM leo ni wazoefu so usiogope.. kingine

HAKUNA MZOEFU BARABARANI LAITI WANGEKUWEPO AJARI ZINGEKUWA HISTORIA TU
 
Msisahau kufaa makoti

Na miwani, kuzuia vumbi na wadudu machoni
Bora umewakumbuka! Kuna ndugu m1 pale kimara baruti zamani kidogo alikua na baja kaiva, hamadi, mdudu wa kutoboa mbao akaingia jichoni! Alipona akawa mlemavu sijui kama yupo nao_deiz
 
Wazee inawezekn nlitoka na Houjue express kutoka mwanza to dodoma masaaa ty ila oil uwe unaweka Castrol ni hatari km 2000 so n mwendooo tuuuu
 
Haya mambo yanawezekana sema inataka ujasiri na umakini tu, chuma hiyo (Sanya) nilitembea nayo Kutoka Mwanza-Shinyanga-Nzega(Tabora)-Singida-Dodoma-Iringa-Mbeya, (maskani moja hiyo) na baada ya Siku 4 nikasogea mpaka Tunduma kumpa hi mshkaji wangu pale boarder.
Nilitoka Mwanza saa Tano asbh nikalala Dom saa moja jioni, asubuhi nikaamsha saa moja asbh saa kumi jioni nikatoboa Mby town.
Safari ya kurudi sikulala njiani ila ndo baridi ya usiku iliniishia no matter mavazi ya kujikinga nilivyojiset yaani motor cycle driving gears kama zote.
In short niliienjoy sana Ile tour ingawa Sina mpango wa kuirudia tena ile kitu aisee, so piga moyo konde hata hiyo 110 Yako ni usafiri tosha kabisha muhimu kuzingatia motorcycle safety and road rules.
Screenshot_20220823-120937.jpg
 
Vp ulishaenda huko tanga ?
Mkuu nilienda na nilifika salama.. kiukweli watu tunatishana sana ila huko barabarani hakuna changamoto kubwa.. changamoto niliyoiona

1. Mashimo ya barabarani
- yana haribu sana pikipiki na kusababisha baadhi ya nati kulegea hivyo inabidi serv ya kukaza

2. speed mwisho cheza 60/70
- kwa sababu break za pikipiki sio rafiki sana ukiwa speed kubwa sababu hapa tunategemea taili moja tena ya nyuma kwa 90% na mbele kwa 10% hivyo ukiwa speed kusimama ni ngumu sana hasa ukiona kitu na kufanya kujiami.

3. zile bumps3
- zile 3 bumps kiukweli zina haribu sana pikipiki yaan unaweza ukaacha nati nyuma so make sure taili zako azijaa sana upepo hasa ya mbele.

4. barabara ndogo
-hapa kiukweli nawapongeza madereva watu wanasema ooh sijui wanakugonga kiukweli ni uongo katika kuendesha kwangu madereva barabara ikiwa ndogo mara nyingi walikuwa wanapunguza mwendo na kunipigia on kuwa nibane.. na kiukweli wanazingatia sana endkat


nitaleta uzi jinsi nilibyoanza safari.. japo nilichoka sana ila nilienjoy.. nilichoka sababu nilifanya makosa ya kubeba beg mgongoni na lilikuwa na laptop
 
Back
Top Bottom