msuyaeric
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 842
- 1,197
- Thread starter
- #41
Aisee pole Sana...Dar- Moro nimeenda mara kibao changamoto ipo maeneo ya uzomozi zone kuna baridi na upepo.
Mwaka jana nimesafiri na pikipiki ya Sanlg choka mbaya toka maeneo ya Usevya nikapita kwenye mbuga ya katavi nikahunga strike,mpanda ,uvinza,kasulu huko kote skikutana na check point wala polisi nilipo fika kibondo sasa kuna kibelia fulani nikikutana na afande mjaluo analazimisha rushwa yaani njaa mbaya baada ya hapo nikaanza kuhitafta buhigwe na Kakonko nafika Kakonko spoketi yote stadi na meno vimeisha fundi akafunga Fasta nihitafte Nyakanazi jioni giza linaingia nikalazamisha kufika Biharamulo ni saa tatu usiku nimejaa vumbi kugoma kuna vumbi balaa nikalala asubuhi saa moja nikaanza safari ya Muleba barabarani nilikua nakutana na manyani yanadharau haya pishi huko kote hakuna usumbufu kama kule kibondo belia ya Biharamulo askari yupo poa sana baadae kasindaga Muleba nikashuka zangu Nshamba nikasalmia then nikahitafta kamachumu ,rubale kufika kasikisi nikagongana na bodaboda bhana safari yangu ya katolo ikawa imefikia hapo nikarudi izibya hospitalini kutibiwa mguu kwanza mafuta na gharama yote haikufikia laki na nusu.
Hii safari ngumu na hinakuhitaji kubwa moyo Mugumu na kutanguliza Mungu
Ukanda huu wa mikoa ya magharibi una mapoli mengi na usiku kuna mambo mengi sio yote naweza sema humu
Baadae pikipiki niliacha nikarudi na basi la ruchoro ya mwanza Sumbawanga
Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app