Pikipiki yangu inachelewa kuwaka

Pikipiki yangu inachelewa kuwaka

baba aura

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2023
Posts
254
Reaction score
393
Habar wakuu,Nina pikipiki aina ya boxer bm 150 inatatizo moja La kuchelewa hasa ikiwa nimeipaki kwa nusu saa hivi,nimejaribu kwenda kwa mafundi ila wamekuwa wanatoa maoni tofauti tofauti.

Nawasha kwa kutumia kick ila kuna mda nafikiria ninunulie motor starter itakuwa suluhisho LA tatizo au laa!? Wakuu naoni yenu muhimu sana

MARAJESHO;
Asanteni sana kwa ushauri wenu kwani kwa namna Fulani umenisaidia sana

Pikpiki imekutwa na tatizo La kufua umeme ,shida inakuja tena ,nawezaje kumaliza tatizo hili?
 
Habar wakuu,Nina pikipiki aina ya boxer bm 150 inatatizo moja La kuchelewa hasa ikiwa nimeipaki kwa nusu saa hivi,nimejaribu kwenda kwa mafundi ila wamekuwa wanatoa maoni tofauti tofauti.
Nawasha kwa kutumia kick ila kuna mda nafikiria ninunulie motor starter itakuwa suluhisho LA tatizo au laa!? Wakuu naoni yenu muhimu sana
Boss acha kupiga kick unashtua viumbe hai waliopo kwenye kende vile una_vibrate kupiga kicks nyingi chuma haiwaki,

Kick start haifai viatu vinaisha, vuta choki piga kick moja isipowaka peleka kaweke motor uwe unatenkenya tu,

nilishakuwa na chopa mpaka nikawa bingwa wa kupiga kicks, halafu kuna addiction hata siku ukishika chuma mpya unapiga kick, muda mwingine fanya kuishtua.
 
Ungeanza na vitu vidogo vidogo kwanza
1. kabadilishe Plagi kama bado;
2. Ikifuatiwa na kuangalia kabureta, huenda inaruhusu mafuta mengi
3. Hakikisha unaweka mafuta safi kutoka kituo cha mafuta na sio yale ya vidumu barabarani , Boxer inachagua mafuta/haitaki mafuta yaliyopita mikono mingi....
Ukishafanya hayo kwa ukamilifu kama bado ina sua sua ndio hatua zingine zifuate
 
Mafund wa boxer n wachache sanaaa....hiyoo boda inaweza kuwa na shda ya plug, wiring, au valve au timing chain imejirusha.....sooo tafuta fund aanze kuangalia kuazia waya wa magneto.. kama unapeleka umeme good ..na kama plug inamwaga moto wa uhakika

Kingne boxer haitak vtu feki...tafuta genuine spare parts...plug weka ya BOSCH..etc...
 
Boss acha kupiga kick unashtua viumbe hai waliopo kwenye kende vile una_vibrate kupiga kicks nyingi chuma haiwaki,

Kick start haifai viatu vinaisha, vuta choki piga kick moja isipowaka peleka kaweke motor uwe unatenkenya tu,

nilishakuwa na chopa mpaka nikawa bingwa wa kupiga kicks, halafu kuna addiction hata siku ukishika chuma mpya unapiga kick, muda mwingine fanya kuishtua.
Sawa mkuu
 
Thanks mkuu but motor za boxer bei gani?
 
Shida haipo kwenye motor starter, labda kama unataka kutumia starter kuwasha, hilo tatizo ni either wiring system, carburettor(fuel floating), valve, ignition coil...nk.
 
Kwa hiyo mkuu hats nikiweka motor mpya tatizo litakuwepo palepale?

Kama kuna shida kwenye mfumo wa kufua umeme, au carburettor au mfumo wa waya, hata ukiweka starter mpya tena original bado tatizo halitaisha.
 
Kwa hiyo mkuu hats nikiweka motor mpya tatizo litakuwepo palepale?
tena kama imeshindwa kuwaka kwa kick usitegemee starter itawasha....itacrank hadi betri liishe

naungana na wadau wanaosema anza na vitu vidogo mf.
Plug, wachunguze mfumo wa mafuta carb, na tank kama kuna uchafu ama changamoto nyingine, ignition coil na magneto na hatimaye valve kama zina carbon hilo tatizo husumbua
 
Kama ishu inatokea baada ya kupaki muda mrefu kacheki carburetor huenda inafloat
 
Back
Top Bottom