Pikipiki yangu!!

Pikipiki yangu!!

Ninoma

Member
Joined
Aug 29, 2021
Posts
9
Reaction score
5
Pole na kazi wakuu!!

Mafundi naomba munisaidie nipo kijijini huku Nina pikipiki aina ya TVS changamoto yake Ni kwamba inasumbua kuwaka. (Napiga kiki mpaka nachoka)(Ukisukuma inawaka) hata ikiwaka ikikaa hata masaa mawilo ina Anza Tena kusumbua kuwaka!! Yaani mpaka iwake Ni changamoto.
Clatch center Ni mpya,

Hizi pikipiki za TVs Ni changamoto kwa kweli.
Hata nikipeleka kwa fundi anaiwasha ikilala tu asubuhi unapiga kiki Zaidi ya 200 ikiamua haiwaki (plug Ni mpya)

Ninachotaka iwe inawaka faster watalamu nisaidie

Nini nibadilishe (nirekebishe)) ili kutatua hii shida!!
 
Pole sana mkuu, Kiki zitakufanya ujazie mguu mmoja...

Hebu cheki afya ya battery na starter motor, zikiwa vizuri basi tatizo litakuwa kwenye compression (valve za pikipiki huwa zinazingua)
 
Yan kabla hujang'amua tatizo ushahitimisha kuwa TVS ni changamoto!
 
Hii pikipiki naitumia kuanzia 2018 sijawahi kupata hizo shida,hapo tatizo linaweza kuwa betri,ila ni pikipiki ngumu Sana ila mafundi wengi waliozoea hizi za kichina wanaziharibu
 
Back
Top Bottom