Mkuu Inteli, mimi ni bike lover and at one time nilikuwa namiliki 5 big bikes, sasa japo siendeshi tena, lakini bado namiliki bikes 2, off road na on road.
- Big Bikes are expensive, Bei zina range from US $ 6,000 hadi 18,000 depending on brand and status.
- Bongo hakuna dealers wa big bikes, mahali pa karibu ni South ila ghali, bali kuna watu wachache wanaoleta big bikes ila siku hizi sizioni, na mara moja moja hutokea wazungu wakaziuza bikes zao matangazo unaweza kuyaona sehemu za wazungu wazungu, Slip way, Shoppers etc, Mlimani City etc. Njia rahisi na bei rahisi hivyo the best option ni kuagiza kama wanavyoagiza magari.
- Hakuna spares za big bikes bongo, bali ukinunua Honda CBX 750 na BMW 750 unaweza kupata spares kwenye karakana ya polisi, Kilwa Rd (maafande wanakuibia!), chini ya hapo ni kuagiza tuu and it takes 3 days kwa spares from South, 5 days ukiagiza toka Dubai, 14 days ukiagiza toka Japan.
- Kwa vile hakuna show window ya big bikes bongo pia hakuna authorised dealers wala services, ila kuna mafundi wa bongo wanatumia tuu undundu kufungua bike ya aina yoyote, mmoja wa jamaa wazuri sana anaitwa Amiri yuko pale Magomeni Mikumi mkono wa kulia kuelekea Kigogo.
- Big bikes ziko imara sana, my last bike niliopata nayo ajali, ni Harley Davidson Buell Thunderbold 1100cc, niliinua US na nimekaa nayo 2 years haikuwahi hata kupata pancha!, speed ni 240kmh. Dar-Moro natumia 1:45 hrs, Dar-Dodoma 3:45 hrs, Dar-Arusha 5 hrs!.
NB. Angalizo, kwanza Tanzania hatuna barabara za big bikes hivyo the risk is too big!. Wenzetu wan a bike lane kwenye barabara zap hivyo cross country is safe.
Pili madereva wetu wa magari sio makini kivile kwenye long distance, hivyo you have to be extra extra careful.
Pasco