Pikipiki za masafa marefu (Cross countries)

Pikipiki za masafa marefu (Cross countries)

The Intelligent

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2013
Posts
2,459
Reaction score
824
1601459159226.png


Wakuu anayefahamu aina hizo za pikipiki anijuze nahitaji kununua.
Ni pikipiki kubwa kimuundo na ni nene, pembeni nyuma huwa na kitu kama begs ngumu. Mara nyingi nawaona nazo raia wa kigeni hasa wanaotokea South Africa.
Ni pikipiki zenye kasi ya ajabu sana. Naomba kujua hizo pikipiki kama ifuavyo;-
1. Bei yake ya kuinunua
2. Mahali zinapouzwa hapa tz
3. Upatikanaji wa spare parts
4. Mafundi wake
5. Uimara wake/ nchi zinakotoka
Natanguliza shukrani.

MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU
Mkuu Inteli, mimi ni bike lover and at one time nilikuwa namiliki 5 big bikes, sasa japo siendeshi tena, lakini bado namiliki bikes 2, off road na on road.

  1. Big Bikes are expensive, Bei zina range from US $ 6,000 hadi 18,000 depending on brand and status.
  2. Bongo hakuna dealers wa big bikes, mahali pa karibu ni South ila ghali, bali kuna watu wachache wanaoleta big bikes ila siku hizi sizioni, na mara moja moja hutokea wazungu wakaziuza bikes zao matangazo unaweza kuyaona sehemu za wazungu wazungu, Slip way, Shoppers etc, Mlimani City etc. Njia rahisi na bei rahisi hivyo the best option ni kuagiza kama wanavyoagiza magari.
  3. Hakuna spares za big bikes bongo, bali ukinunua Honda CBX 750 na BMW 750 unaweza kupata spares kwenye karakana ya polisi, Kilwa Rd (maafande wanakuibia!), chini ya hapo ni kuagiza tuu and it takes 3 days kwa spares from South, 5 days ukiagiza toka Dubai, 14 days ukiagiza toka Japan.
  4. Kwa vile hakuna show window ya big bikes bongo pia hakuna authorised dealers wala services, ila kuna mafundi wa bongo wanatumia tuu undundu kufungua bike ya aina yoyote, mmoja wa jamaa wazuri sana anaitwa Amiri yuko pale Magomeni Mikumi mkono wa kulia kuelekea Kigogo.
  5. Big bikes ziko imara sana, my last bike niliopata nayo ajali, ni Harley Davidson Buell Thunderbold 1100cc, niliinua US na nimekaa nayo 2 years haikuwahi hata kupata pancha!, speed ni 240kmh. Dar-Moro natumia 1:45 hrs, Dar-Dodoma 3:45 hrs, Dar-Arusha 5 hrs!.
NB. Angalizo, kwanza Tanzania hatuna barabara za big bikes hivyo the risk is too big!. Wenzetu wan a bike lane kwenye barabara zap hivyo cross country is safe.

Pili madereva wetu wa magari sio makini kivile kwenye long distance, hivyo you have to be extra extra careful.

Pasco
---
Kwa anayetaka kukosha macho juu ya madude ya ukweli ninayo yazimika aone japo kw aufupi tu...ndo utajua tofautit kati ya boda boda na vyombo vya wanaume.

1..Harley davidson motorbikes
2.bmw motorbikesView attachment 171220View attachment 171221View attachment 171222View attachment 171223View attachment 171224View attachment 171225
---
Huo upande BMW ni monsters View attachment 1584184

Jipange kuanzia 25m

Ila mimi huwa nakubali sana off road bike za Yamaha na HondaView attachment 1584185
 
Amewahi kuzituia kama sikosei na alikuwa anaishi dar na kufanya kazi moro na alikuwa anawahi kila siku kwa type hiyo kama kumbu kumbu zipo sawa.

Aisee! ndio nahitaji kitu kama hicho cha masafa ya ukweli.
 
Amewahi kuzituia kama sikosei na alikuwa anaishi dar na kufanya kazi moro na alikuwa anawahi kila siku kwa type hiyo kama kumbu kumbu zipo sawa.

Nadhani tupo sawa kwa kumbukumbu mkuu.
 
BMW K-1600 GTL au Harley Davidson ni nzuri mno. Ila ni mpaka uagize nje,,mpya ni dola 25,000. Used unapata hadi dola 10,000. 1740cc,,na 1600cc ni gari la miguu muwili hilo mkubwa. Unaendesha ukiwa umevaa vifaa maalum.
 
Google ; Harleydavidson na BMW motorbikes kuanzia 750cc utakutana nazo!!!!
 
BMW K-1600 GTL au Harley Davidson ni nzuri mno. Ila ni mpaka uagize nje,,mpya ni dola 25,000. Used unapata hadi dola 10,000. 1740cc,,na 1600cc ni gari la miguu muwili hilo mkubwa. Unaendesha ukiwa umevaa vifaa maalum.

Na spea zake vipi mkuu?
 
Na spea zake vipi mkuu?

Kumanage hiyo pikipiki unahitaji uwe na hela mkubwa. Zambia-Lusaka ndipo niliwahi liona duka kubwa la vifaa vya pikipiki aina hiyo,ila ukiinunua kama ni mpya utaanza gusa injini baada ya miongo/decades kadhaa.

Ni pikipiki haswaa sio. Pia kuna ya kijerumani inaitwa MZ mzee mmoja alikw nayo imekatika piston basi imepaki miaka kibao.
 
Kaka hii speed ya meter 180/h sio ndogo sana au macho yangu?

Km 3 kwa dakika sio spidi ya mchezo Malila. Ukitoka Dar mpaka Durban (4093 km) South Africa utaenda kwa masaa 22 tuu kwa speed hiyo.
 
Km 3 kwa dakika sio spidi ya mchezo Malila. Ukitoka Dar mpaka Durban (4093 km) South Africa utaenda kwa masaa 22 tuu kwa speed hiyo.

Hebu weka speed calculation hapa wengine hesabu zinatupiga chenga.
 
Back
Top Bottom