Pilipili ina raha gani?

Pilipili ina raha gani?

Kuna muhindi nilikutana nae Mwanza akitaka kupima pilipili Kama ni Kali ,anaikata anasugulia kwenye jicho.
Wenu mtiifu,
Mwalimu wa muziki na mapenzi.
hahahahahaha[emoji51][emoji27]
 
Kuna muhindi nilikutana nae Mwanza akitaka kupima pilipili Kama ni Kali ,anaikata anasugulia kwenye jicho.
Wenu mtiifu,
Mwalimu wa muziki na mapenzi.

Kkkkkk
Kuna mashindano huko India ya kula pilipili na pia yapo ya kusugua kwenye macho na kuna siku mwanamke alichukua ushindi maana alisigina pilipili machoni bakuli zima halafu pilipili mbuzi

Ethiopia wao wanaloweka nyama mbichi kwenye sufiria lililojaa pilipili halafu wanaweka juani mpaka inaiva yenyewe halafu wanakula

Kuna watu wanapenda pilipili aisee

Mimi chakula bila pilipili naagiza sokoni
 
Nilikuwa sili kwakuwa nafanya mazoezi. Kutokana na kutoila muda mkubwa hata baada ya kuacha mazoezi mpaka leo situmii pilipili.
Mimi nakula sana ila nikiwa nafanya mazoezi niligundua kama inanichoma(kichomi)sijui ndiyo tatizo pilipili ?

M2anzo nilidhani kwa sababu nakunywa maji nefore mazoezi
 
Umenikumbusha kuna siku nikarishwa chakula wanigeria, asee nijuta.

Wale jamaa nao wanapenda sana pilipili.
Ukiwa huko lazima utapata ulabu wa Pilipili hasa kama sie miaka hiyo ya 80s imagine tulipiga kitabu miaka miwili. Ilikuwa hakuna jinsi halo Lagos, ila mwenzangu Nadhani ulijitahidi usile konokono maana nasikia ukila konokono lazima uanze kuuza nganda
 
Japo sijawahi kufika huko kwao kabisa, ila kuna mazingira nilipata kuishinao, ingawa hii ya kula konokono sijawahi kulisikia kwa hawa.
Ila hawa wanatabia ya kula ngozi, halafu huwa wanaiweka muda mrefu au hata nyama unakuta wanaiweka muda mrefu hadi inatoa harufu.

Yaani ni mambo ya kustaajabisha sana.
 
Ukiachana na faida za kiafya. Pilipili inaongeza hamu ya kula. Pilipili ilivyo tamuuu mimi napenda pilipili uwiiii. Kwenye chai inabid nijaze black pepper ili ninywe.
Weka na tangawizi nyingi. Ule muwasho wake sasa. Unaweza kunywa chai chupa nzima. Mie siku hizi mpk chakula cha mchana nakunywa na chai. Na nikikosa pilipili nakuwa kama teja [emoji24]
 
Dah basi we chakula changu hugusi, mimi nakula pilipili inafika wakati siisikii kabisa, kwenye mboga uwa naweka hadi kumi
 
Nyama Choma au Nyama Kavu yoyote ninapoila Lazima pembeni niwe na Mixer hii hapa Chini

Mahitaji

Pilipili za kuwasha kweli kweli 3 au 4
Malimao makubwa mazuri ma 2
Chumvi kidogo tu

Maandalizi

Kata pilipili ndogo ndogo sana unachop vyema kbsa vnakua vidogoo

Unakamulia yale malimao mawili makubwa maji yake kwenye hizo pilipili

Unasiginia vizuri kabisa maji yasipotosha unaongeza limao 1 na pilipili 1

Unanyunyizia chumvi kwenye hako kamchanganyiko chako,kazi inaishia hapo.

Tonge 1 la ugali nyama unachovya kwenye hiyo mixer,Uamuzi ni wako uchovye

nyama kwenye mixer u uchovye tonge la ugali,Mimi kwakua n mkombaji pilipili

huwa nachovya nyama, kisha ugali unend dry mdomoni,NI MOJA ya kiungo changu

pendwa sana wakati nakula,Kama hamna malimao sio mbaya pilipili nikishka mkononi

nikiwa naitafuna yenyewe kama yenyewe huku nikiw nachakula changu pembeni.

Msosi usio washa Bado haujakamilika,pilipili ndio Kila kitu kwenye misosi yangu.
 
Chai pia Tangawizi iwe ya kutosha, Pilipili Manga pia kiaina

Unakunywa chai inawashaaa yani kajasho kanatoka tu chenyewe,Amaizing sana.
 
Huwa nashangaaga hadi wanaume hawali pilipili na hawana matatizo ya kiafya
 
Nyama Choma au Nyama Kavu yoyote ninapoila Lazima pembeni niwe na Mixer hii hapa Chini

Mahitaji

Pilipili za kuwasha kweli kweli 3 au 4
Malimao makubwa mazuri ma 2
Chumvi kidogo tu

Maandalizi

Kata pilipili ndogo ndogo sana unachop vyema kbsa vnakua vidogoo

Unakamulia yale malimao mawili makubwa maji yake kwenye hizo pilipili

Unasiginia vizuri kabisa maji yasipotosha unaongeza limao 1 na pilipili 1

Unanyunyizia chumvi kwenye hako kamchanganyiko chako,kazi inaishia hapo.

Tonge 1 la ugali nyama unachovya kwenye hiyo mixer,Uamuzi ni wako uchovye

nyama kwenye mixer u uchovye tonge la ugali,Mimi kwakua n mkombaji pilipili

huwa nachovya nyama, kisha ugali unend dry mdomoni,NI MOJA ya kiungo changu

pendwa sana wakati nakula,Kama hamna malimao sio mbaya pilipili nikishka mkononi

nikiwa naitafuna yenyewe kama yenyewe huku nikiw nachakula changu pembeni.

Msosi usio washa Bado haujakamilika,pilipili ndio Kila kitu kwenye misosi yangu.
Daah hadi mate yamenidondoka

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
mi chai isiyo na limao sinywi,
chakula chochote kisicho na pilipili sili!
 
Pilipili inaongeza ladha ya chakula pia no dawa ya maradhi.
Mimi nakula Sana pilipili ila sio Kama wachina na wahindi wale komesha
 
Back
Top Bottom